KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Monday, December 23, 2013

DAR MODERN TAARAB KUZINDUA UKUMBI WAKE


KIKUNDI cha muziki wa taarab cha Dar Modern kinatarajia kuzindua ukumbi wake mpya wa burudani hivi karibuni.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikundi hicho zimeeleza kuwa, ukumbi huo umejengwa katika maeneo ya Magomeni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa habari hizo, uzinduzi wa ukumbi huo utakwenda sambamba na onyesho kabambe litakalofanywa na kikundi hicho.

Wednesday, November 6, 2013

VIKUNDI VYA TAARAB VYAUNDA UMOJA



HATIMAYE wasanii na viongozi wa vikundi vya taarab nchini, wameamua kuanzisha
umoja kwa lengo la kuzungumzia matatizo yao.

Lengo lingine la kuanzishwa kwa umoja huo ni kutetea maslahi yao na kupanga
mikakati ya kupanua soko la muziki huo.

Mkurugenzi wa kundi la East African Melody, Ashraf Mohamed amesema
wanatarajia kukutana hivi karibuni kuzungumzia matatizo yao.

Ashraf alisema wamefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa, vikundi vyao
vimekuwa vikitumika kuwanufaisha watu wengine.

Amesema wakati wasanii wamekuwa wakiumia vichwa kutunga, kuimba na kupiga
nyimbo nyingi za taarabu, wanaonufaika ni wajanja wengine.

"Tunadhani huu ni  wakati wa bendi za taarab kujiendesha kibiashara kwani makosa
tunayoyafanya sisi viongozi, yanawaumiza sana wasanii wetu, hivyo ni bora tuamke
ili tupange mambo yetu kwa pamoja,"amesema.

Kiongozi huyo amesema japokuwa wamechelewa kuchukua uamuzi huo, lakini
wanao muda wa kutosha wa kuweza kurekebisha mwenendo na mwelekeo wao.

FIVE STARS SASA KUITWA VIP MODERN TAARAB



UONGOZI wa kikundi cha taarab cha Five Stars, umeamua kubadili jina la kundi hilo
na kujiita VIP Modern Taarab.

Habari kutoka ndani ya kundi hilo zimeeleza kuwa, uamuzi huo umelenga kubadili
mwelekeo na kukifanya kikundi hicho kiwe na mwelekeo mpya.

Hata hivyo, viongozi wa kundi hilo hawakuwa tayari kusema lolote kuhusu uamuzi
huo kwa vile jambo hilo limefanywa kuwa siri kubwa.

Lakini habari za uhakika zimeeleza kuwa, tayari uongozi umeshalipitisha jina hilo na
baadhi ya wadau wa taarab wamelisifu kwa madai kuwa ni zuri.

Kundi la Five Stars lilijipatia sifa kubwa wakati lilipoanzishwa kutokana na kuibuka na
vibao vyenye mvuto, ambavyo viliwapa homa viongozi wa vikundi vingine.

Thursday, October 24, 2013

KHADIJA KOPA: NARUDI UPYA NA MAMBO MAPYA



HATIMAYE mwimbaji nyota wa nyimbo za muziki wa taarab nchini, Khadija Omar Kopa amemaliza eda na anatarajiwa kurudi ulingoni Oktoba 30 mwaka huu.

Khadija, ambaye alifiwa na mumewe Juni mwaka huu, alimaliza eda wiki iliyopita nyumbani kwa mumewe, Bagamoyo mkoani Pwani.

Mwanamama huyo kwa sasa amerejea nyumbani kwake Mwananyamala, Dar es Salaam, ambako ndiko alikokuwa akiishi kabla ya kuolewa.

Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Khadija alisema amealikwa kufanya onyesho maalumu Oktoba 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Villa Park ulioko Mwanza.

Khadija alisema baada ya onyesho hilo, atapanda tena stejini Novemba 3 mwaka huu katika onyesho litakalofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live ulioko Mbagala mjini Dar es Salaam.

Alisema baadhi ya mashabiki wake wameandaa onyesho la Dar Live kwa lengo la kumchangia kutokana na msiba mzito alioupata wa kufiwa na mumewe.

Mume wa msanii huyo, Jaffari Ali Yusuf alifariki dunia nyumbani kwake Bagamoyo baada ya kuugua kwa muda mfupi na kuzikwa huko huko.

Kutokana na kifo hicho cha mumewe, Khadija alilazimika kuacha kufanya maonyesho ya taarab ili kukaa eda kwa miezi minne kwa mujibu wa taratibu za kisheria za kiislamu.

Khadija amewashukuru wakazi wa Bagamoyo kwa kumpa ushirikiano wa hali ya juu katika muda wote aliokuwa akiishi na mumewe katika wilaya hiyo ya kihistoria.

Malkia huyo wa mipasho alisema, baada ya kufiwa na mumewe, amegundua kwamba anapendwa na watu wengi tofauti na alivyokuwa akifikiria.

Khadija alisema kipindi chote alichokuwa kwenye matatizo, alishangazwa na ukaribu ulioonyweshwa na watu, ambao hakuwatarajia na ameijua nafasi yake kwenye jamii.

 “Nimesaidiwa na asasi mbalimbali, vikundi pamoja na watu wengi na wengine walikuwa wakiniambia nikitaka msaada, niwapigie ingawa sijafanya hivyo. Nimefarijika sana kuona napendwa kiasi hiki,” alisema mwanamama huyo, ambaye alimaliza eda Oktoba 16, mwaka huu.

Alisema itamchukua muda kidogo kuweza kupanda tena jukwaani kutokana na hali aliyonayo na kuongeza kuwa, anataka atakapotoka, aonekane mtu mpya na mwenye mambo mapya.

Kwa mujibu wa Khadija, katika onyesho lake la kwanza, anatarajia kutoka na wimbo mpya, unaojulikana kwa jina la Mwanamke kujiamini.

Alisema alitunga wimbo huo kabla ya kifo cha mumewe, lakini alichelewa kuutoa kutokana na kutingwa na mambo mengi.

"Nataka kwanza nitulize akili yangu. Namuomba Mungu anirejeshee nguvu upya ili nikitoka, nitoke kivingine,"alisema mwimbaji huyo wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT).

Khadija, ambaye ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM alisema, baada ya onyesho la Dar Live, anatarajia kufanya onyesho lingine la kuwaaga wakazi wa Bagamoyo.

"Onyesho hili litakuwa maalumu kwa ajili ya kuwaaga wakazi wa Bagamoyo kutokana na kuishi nao vizuri muda wote niliokuwepo hapa na mume wangu,"alisema mwanamama huyo.

Khadija alisema anamshukuru Mungu kuona kuwa, bado yuko imara na amewaomba mashabiki wake, wamuombee dua ili aweze kurudi upya.

"Hii ni kazi yangu inayoendesha maisha yangu na ya familia yangu, nataka nitakaporudi ulingoni, niwe mpya, nitoke angalau na nyimbo mbili mpya, nawaomba mashabiki wangu waniombee kwa Mungu ili nirudi upya,"alisema.

Khadija alisema katika maonyesho hayo, anatarajia kuimba nyimbo zake mpya na za zamani na kuwaomba mashabiki wampokee kwa mikono miwili.

"Unajua ukiwa kwenye eda, unarudi nyuma sana, hivyo nahitaji muda kidogo wa kupanga mambo yangu upya ili nijue nitatoka vipi,"alisema mwimbaji huyo, ambaye aliwahi kung'ara kwa vibao vya Daktari, Wahoi na Kadandie wakati alipokuwa kikundi cha Culture cha Zanzibar.


Sunday, September 29, 2013

MWASITI AJIENGUA TOT PLUS



Mwasiti Suleiman (kulia) akiwa na waimbaji wenzake wa TOT katika moja ya maonyesho ya kikundi hicho.

MWIMBAJI Mwasiti Suleiman wa kikundi cha taarab cha Tanzania One Theatre (TOT Plus) ameamua kujiengua katika kikundi hicho.

Mwasiti amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa, ameamua kujiengua TOT Plus kwa sababu ya maslahi duni.

Amesema amekuwa akifanyakazi katika kikundi hicho kwa zaidi ya miaka tisa na kuongeza kuwa, hakuwahi kuajiriwa zaidi ya kufanyakazi kama kibarua.

Amesema katika miaka miwili ya kwanza, hakuwa akilipwa chochote na kwamba katika miaka saba iliyofuata, alikuwa akilipwa posho.

Mwasiti amesema kwa sasa ameamua kufanyakazi katika kampuni moja ya Wakorea, ambayo hakutaka kuitaja, lakini pia amekuwa akijihusisha na muziki huo katika vikundi vya mitaani.

Mwanadada huyo amesema haoni tofauti yoyote katika maisha yake ya sasa na wakati alipokuwa akifanyakazi TOT Plus na kwamba muziki haikuwa ajira pekee ya kuendesha maisha yake.

"Nilipo naweza hata kuuza vitumbua au maandazi kwa sababu zote ni kazi. Kila siku tunapishana na akina mama wakifanyakazi mbalimbali na wanaishi,"amesema mwanamama huyo mwenye mwanya wa kuvutia.

Alisema hakuwahi kugombana na mtu yoyote kwa kipindi chote alichokuwa TOT Plus na kwamba aliwaaga viongozi wake huku akiwaeleza wazi kwamba maslahi duni ndiyo yaliyomkimbiza.
Amesema anaweza kuwa tayari kurudi katika kikundi hicho iwapo tu atahakikishiwa ajira na maslahi mazuri.

Mwanadada huyo amesema pia kuwa, yupo tayari kujiunga na kikundi kingine cha taarab iwapo kitamuhakikishia ajira na maslahi mazuri.

Friday, September 27, 2013

MZEE YUSUPH KUSTAAFU MUZIKI 2015


MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab nchini, Mzee Yusuph amesema anatarajia kustaafu kazi hiyo katika kipindi cha miaka miwili ijayo.

Mzee, ambaye ni kiongozi wa kikundi cha Jahazi. amesema uamuzi wake huo umelenga kuwapa nafasi vijana kuonyesha vipaji vyao.

"Ni vigumu sana kuacha muziki wakati kikundi chako kipo juu, lakini kwa kuwa nimeshaamua, lazima nitekeleze hilo,"amesema Mzee alipozungumza na blogu ya

"Sina muda mrefu mbele, nitaweka kipaza sauti pembeni ili kuwapisha vijana waendeleze tasnia hii,"aliongeza.

Mtunzi na mwimbaji huyo mwenye sauti yenye mvuto, amesema uamuzi wake huo unaweza kuwaumiza mashabiki wake, lakini hana lingine la kufanya zaidi ya kuutekeleza.

"Kwangu mimi ni maamuzi magumu sana kwa vile nitakiacha kitu ninachokipenda na mashabiki wamenizoea, lakini itabidi wakubaliane na maamuzi haya,"alisema mwimbaji huyo, ambaye pia amepachikwa jina la Mfalme.

Kwa mujibu wa msanii huyo, baada ya kustaafu muziki, atalazimika kukivunja kikundi chake cha Jahazi na kumpatia kila msanii haki anayostahili kwa ajili ya kuendeleza maisha yake.

"Ningependa wasanii nitakaowaacha, watafute bendi zingine za kufanyakazi kwa kipindi hicho ili waendelee kuimba na kukuza zaidi vipaji vyao,"alisisitiza.

THABITI ABDUL AMWACHA SOLEMBA ISHA MASHAUZI


MKURUGENZI msaidizi wa kikundi cha taarab cha Mashauzi Classic, Thabiti Abdul amejiengua katika nafasi hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kundi hilo zimeeleza kuwa, Thabiti ameshawasilisha barua ya kujitoa kwenye  kundi hilo kwa mkurugenzi wake, Isha Mashauzi.

Hata hivyo, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Abdul au Isha kuhusu uamuzi wake huo.

Thabiti ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi la Five Stars Modern Taarab, lakini amekuwa akishiriki mara kwa mara kwenye maonyesho ya Mashauzi Classic.

Hivi karibuni, Isha alikaririwa akisema kuwa, Thabiti bado yupo kwenye kundi hilo na amekuwa akishiriki kwenye maonyesho mbalimbali.

Habari kamili kuhusu uamuzi huu utazipata hivi karibuni kupitia kwenye blogu yako ya Rusha Roho.

ISHA: SIPENDI KUUMIZWA KIMAPENZI


KIONGOZI wa kikundi cha muziki wa taarab cha Mashauzi Classic, Isha Mashauzi amesema kamwe katika maisha yake hapendi kuumizwa kimapenzi na mwanaume.

Isha amesema anapoachana na mwanaume, huwa hageuki nyuma na kwamba mapenzi kwake ni kitu cha kupita.

"Nikiacha nimeacha, sipendi kuumizwa, kazi yangu mwenyewe inaumiza,"alisema Isha alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Ng'aring'ari kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Clouds TV mwishoni mwa wiki iliyopita.

Isha amesema amewahi kutongozwa na wanaume wengi, lakini kutokana na msimamo alionao kimapenzi, wamebaki kuwa rafiki zake baada ya kuwaeleza ukweli wa mambo.

"Wapo zaidi ya wanaume wanne, ambao walinitongoza na kunitaka kimapenzi, lakini niliwaeleza wazi kwamba, kwa vile kila mmoja ana mkewe nyumbani, siwezi kujihusisha nao katika suala hilo. Hivi sasa ni rafiki zangu wakubwa, huwezi kuamini,"alisema.

Hata hivyo, Isha ametahadharisha kuwa, mwanamke anapoamua kumtolea nje mwanaume, anapaswa kuwa makini ili kuepuka kujiingiza katika matatizo.

Alisema wapo wanaume wanaopenda vibaya na wanaoweza kufanya lolote pale wanapokataliwa kimapenzi, ikiwa ni pamoja na kuua ama kujiua.

"Hata kama humpendi, mchukulie taratibu, usimweleze kwa pupa, wewe ni mwanadamu, siyo ng'ombe, hujui anakupenda vipi,"alisema mwanamama huyo, ambaye alianza kupata umaarufu katika muziki wa taarab alipokuwa kundi la Jahazi.

Isha amekiri kuwa, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Jumanne Tevez, ambaye alipiga naye picha za video ya wimbo wake wa Nakupenda kwa dhati, lakini hawakuwahi kupata mtoto.

Anasema anajuta kumtambulisha Tevez kwa watu wengine kwa sababu baadhi yao walitumia nafasi hiyo kumtaka kimapenzi kwa lengo la kumkomoa.

Licha ya kuachana na Tevez baada ya mpenzi wake huyo wa zamani kuoa mwanamke mwingine, Isha amesema bado wanaendelea kuwasiliana na kuwa na urafiki wa kawaida.

"Hata mkewe tuna uhusiano mzuri na wakati mwingine huwa tunapigiana simu kujulikana hali, namwita wifi naye ananiita wifi,"alisema Isha.

Isha amesema katika maisha yake, kamwe hawezi kupigana na mwanamke mwenzake kwa ajili ya kugombania mapenzi. Alisema tabia hiyo imepitwa na wakati.

Ametoa mwito kwa wanawake wa Kitanzania kujenga utamaduni wa  kupendana na kukosoana badala ya kujengeana chuki bila ya sababu za msingi.

Amesema inapendeza mwanamke anapomuonea mwenzake wivu wa kimaendeleo kwa kufanya kile kilichomvutia kutoka kwa mwenzake hata kama atakuwa anamuiga.

Isha amesema licha ya mkurugenzi mwenzake wa Mashauzi Classic, Thabiti Abdul kuhamia kundi la Five Stars, bado amekuwa akiendelea kufanya maonyesho na kundi hilo.

"Thabiti bado tuko naye, anakuja mazoezini, anapiga kinanda na gita kwenye maonyesho, kwa ujumla bado tuko naye,"alisema.

Isha amesema kwa sasa kundi lake la Mashauzi Classic linajiandaa kuipua albamu mpya, itakayokuwa na nyimbo sita. Amesema albamu hiyo itajulikana kwa jina la Asiyekujua hakuthamini.
Albamu hiyo itakuwa ya pili kwa Mashauzi Classic tangu kundi hilo lilipoanzishwa miaka miwili iliyopita.

Albamu ya kwanza inajulikana kwa jina la Si bure una mapungufu, iliyofuatiwa na Viwavi Jeshi. Albamu hizo mbili zilikuwa na nyimbo nne kila moja.

Tuesday, September 17, 2013

MWIMBAJI AHMED MGENI WA ZANZIBAR STARS AFARIKI DUNIA



MWIMBAJI  wa kikundi cha taarabu cha Zanzibar Stars, Ahmed Mgeni, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa ndugu wa marehemu, alisema Mgeni alifariki jana saa kumi na mbili asubuhi katika hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na kichwa na alianza kuugua tangu mwezi wa nne mwaka huu lakini baadae alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Alisema, hali ya marehemu ilibadilika ghafla juzi na kukimbizwa hosipitali kabla ya mauti kumfika na kusema alizikwa jana katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Zanzibar.

Akiwa na kundi la Zanzibar Stars, marehemu aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali na mapema mwaka huu alianzisha kundi lake la muziki wa taarabu lililoitwa Nia Njema.

Thursday, August 8, 2013

FIVE STARS, MASHAUZI CLASSIC, DAR MODERN TAARAB KUTOA BURUDANI IDD EL FITR


Mwanahawa Ally-Five Stars
Isha Mashauzi-Mashauzi Classic
Mwimbaji wa Dar Modern Taarab

KUMBI mbalimbali za burudani za mjini Dar es Salaam kesho na keshokutwa zinatarajiwa kuwaka moto wakati vikundi mbalimbali vya taarab vitakapofanya maonyesho ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Fitr.

Kikundi cha taarab cha Five Stars kitasherehekea sikukuu hiyo siku ya Idd Mosi kwa kufanya onyesho katika kitongoji cha Kigogo Fresh kilichopo Pugu, Ilala, Dar es Salaam.

Kiongozi wa kundi hilo, Ally J alisema juzi kuwa, siku ya Idd Pili, kundi hilo litatoa burudani kwenye ukumbi wa Roshi Garden ulioko Mwandege, Mbagala, Dar es Salaam wakati siku ya Idd Tatu itahanikiza maraha Kibiti, Rufiji mkoani Pwani.

Ally J alisema katika maonyesho hayo, kundi hilo litatambulisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Habari ya mjini.

Kundi la muziki wa taarab la Dar Modern litasherehekea siku ya Idd Mosi kwa kushusha burudani nzito kwenye kiota kipya cha maraha kinachojulikana kwa jina la Serengeti Golden Paradise Resort, Mbagala, Mbande, Dar es Salaam.

Meneja wa hoteli hiyo, Wambura  Sungura alisema juzi kuwa, kundi hilo limeahidi kuporomosha vibao vyake vipya zaidi ya vitano, vitakavyokuwemo kwenye albamu yao mpya.

Sungura amewataka wakazi wa Mbagala na vitongoji vya jirani kufika kwa wingi kwenye ukumbi huo ili kupata burudani adhimu kutoka katika kundi hilo, ambalo lilikuwa kimya kwa zaidi ya miezi miwili.

Kwa mujibu wa Sungura, kabla ya burudani hiyo, kutakuwepo na onyesho ya utangulizi la muziki wa disco kwa ajili ya watoto. Alisema onyesho hilo litaanza saa sita mchana na kuhitimishwa saa kumi na moja jioni.

Kundi la Mashauzi Classic linaloongozwa na Isha Mashauzi limeamua kukwea basi kwenda Morogoro kuwapa burudani ya kusherehekea sikukuu hiyo mashabiki wake katika kitongoji cha Mji Mpya.

Mashauzi alisema juzi kuwa, siku ya Idd Pili kundi hilo litahamishia burudani zake kwenye ukumbi wa City Pub mjini Mbeya wakati Iddi Tatu litamwaga lazi kwenye ukumbi wa Garden Park ulioko Mafinga mkoani Iringa.

Katika maonyesho hayo, Mashauzi alisema kundi hilo litatambulisha nyimbo zake nne mpya, zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu yao mpya, itakayokuwa na nyimbo sita.

Alizitaja nyimbo hizo, watunzi wakiwa kwenye mabano kuwa ni Asiyekujua hakuthamini (Isha na Saida), Bonge la bwana (Hashim Said), Ropokeni yanayowahusu (Saida) na Ni mapenzi tu (Zubeda Maliki).

Monday, August 5, 2013

AMIN-T MOTO BADO IPO HAI

MKURUGENZI wa kikundi cha taarab cha T Moto, Amin Salmin amesema kundi hilo bado lipo hai na limezidi kujiimarisha.

Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Salmin alisema wamepanga kuliimarisha kundi lao kwa kuongeza wasanii wengine sita kutoka makundi mbalimbali.

Salmin alisema wasanii hao watatoka katika vikundi vya Jahazi na Kings Modern Taarab, lakini hakuwa tayari kutaja majina yao.

Kwa mujibu wa Salmin, wasanii wanne watatoka Jahazi na wengine wawili kutoka Kings Modern Taarab.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa kundi la G5 taarab, Hamisi Slim amesema kundi lake lipo katika maandalizi ya kuipua nyimbo mpya nne.

Mbali na kupika nyimbo nne, Slim alisema kundi lake linatarajia kuendelea kujiimarisha kwa kuongeza wasanii wawili wapya. Hakuwa tayari kutaja majina yao.

Saturday, August 3, 2013

KHADIJA KOPA: BAADA YA KUFIWA NA MUME WANGU, NIMEGUNDUA NAPENDWA

MALKIA wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Kopa amesema baada ya kufiwa na mumewe kipenzi, Jafari Ally, amegundua kuwa anapendwa na watu wengi tofauti na alivyokuwa akifikiria.
 Akistorisha na mwandishi wetu, Khadija alisema kuwa kipindi alipokuwa kwenye matatizo alishangazwa na ukaribu ulioonyweshwa na watu hata ambao hakuwatarajia na ameijua nafasi yake kwenye jamii.

 “Nimesaidiwa na asasi mbalimbali, vikundi pamoja na watu wengi, huku wengine wakiniambia kuwa nikitaka msaada niwapigie ingawa sijafanya hivyo, nimefarijika sana kuona napenda kiasi hiki,” alisema mwanamama huyo ambaye anatarajia kumaliza eda Oktoba 16, mwaka huu kabla ya kurejea…

Friday, July 19, 2013

KINGS MODERN TAARAB YAJIANDAA KUTOA ALBAMU MPYA



KIKUNDI cha taarab cha Kings Modern kipo katika maandalizi ya kutoa albamu mpya ya nyimbo za taarab.

Wasanii wanaotarajiwa kuibuka na nyimbo mpya kwenye albamu hiyo ni
Aisha Salum Othuman 'Vuvuzela', Salha Abdala, Kibibi Yahaya na Sophia.

Mkurugenzi wa Kings Modern Taarab, Hamis Majaliwa amesema wamejipanga vizuri kuhakikisha kuwa, albamu hiyo inakuwa moto wa kuotea mbali.

"Tunawaomba mashabiki wetu wakae mkao wa kula na kutegemea mambo mazuri na makubwa kutoka kwetu,"alisema.

"Ni album, ambayo italeta gumzo kwa sababu wapenzi wengi wa taarab wamekuwa wakisubiri kusikia wataimba nini hawa wasanii wapya, hasa Aisha Vuvuzela na Salha,"aliongeza.

Kings Modern Taarab kwa sasa inajumuisha wasanii 13 wakiwemo Aisha Othuman,Salha Abdallah, Kibibi Yahaya, Amina Myalu, Sophia,Anif Juma,Mzaka Nudu,Ibrahim Kamungu,Maneno Goma ,Dogras, Hassan Ally na Mrisho Rajab

JUMA MGUNDA 'JINO MOJA WA JAHAZI' AFARIKI



ALIYEKUWA mpiga gita la besi wa kikundi cha taarab cha Jahazi, Juma Mgunda 'Jino Moja' amefariki dunia.

Mgunda alifariki dunia Jumatano iliyopita kwenye hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
Msanii huyo alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo kwa muda mrefu kutokana na kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.

Mgunda alijipatia umaarufu mkubwa katika fani ya taarab kutokana na kupiga gita hilo kwa umahiri mkubwa katika nyimbo za Daktari wa mapenzi.

Katika sehemu ya wimbo huo, kiongozi wa Jahazi, Mzee Yusuph anasikika akimtaja kwa majina ya 'Juma Mgunda Jini Moja.'

Marehemu Mgunda alizikwa jana katika makaburi ya Tandika, Dar es Salaam.

Wednesday, June 12, 2013

MASHAUZI AFUTIWA MASHITAKA


Na Sylvia Sebastian,DSJ 
MWIMBAJI nyota wa taarabu nchini, Isha Ramadhani, maarufu kwa jina la Isha Mashauzi, ameachiwa huru na Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake bila kuacha shaka.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Matrona Luanda baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake na Mashauzi na mshitakiwa mwenzake, Halima Shaaban kutoa utetezi wao.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Matrona alisema kuwa mahakama hiyo inawaachia huru Mashauzi na Halima, ambao walikuwa wakikabiliwa na shitaka la wizi wa mkoba uliokuwa na fedha taslim sh. 758,200 mali ya muuza duka Sarah Peter.
Alisema kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa bila ya kuacha shaka yoyote.
Mashauzi na mwenzake, walikuwa wakidaiwa kutenda kosa hilo, Aprili 20, mwaka huu, mtaa wa Mafia na Jangwani, walipoingia dukani kwa ajili ya kununua nywele bandia.
Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Sarah ambaye ni muuza duka la Veronica Taki, alidai kuwa washitakiwa waliingia dukani siku hiyo ya tukio saa moja kasoro usiku, ambapo walifanikiwa kuchukua pochi iliyokuwa na fedha hizo ambazo ni za mauzo ya siku.

Monday, June 10, 2013

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA KHADIJA KOPA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia na ndugu jamaa wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri kuu taifa CCM  Hadija Koppa kufuatia  kifo cha mumwewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam.Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo  Ahmed Kipozi na kulia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa CCM Bwana Ridhwani Kikwete(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Koppa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumwewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita.

Friday, June 7, 2013

KHADIJA KOPA ALIVYOUPOKEA MSIBA WA MUMEWE



Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege
 msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania, Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa
 ndege wa mpanda baada ya  kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri  kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimisho ya
 siku ya Mazingira Duniani kitaifa  yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto)akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo Bi Khadija Kopa alikua kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.

Thursday, June 6, 2013

BREAKING NEWSSSS...KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE



Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

Thursday, May 16, 2013

ISHA MASHAUZI ALIKATAA KUPEKULIWA-SHAHIDI


SHIHIDI wa kwanza katika kesi ya wizi wa fedha inayomkabili msanii wa muziki wa taarabu, Isha Mashauzi, amedai kuwa msanii huyo aliingia sehemu ya ndani ya duka hilo na kuchukua pochi yenye fedha.

Akitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Matrona Luanda, shahidi huyo, Veronika Taki, alidai Isha aliingia dukani ambapo haparuhusiwi bila ruhusa yake na kukaa katika kiti cha mmiliki wa duka karibu na boksi ambalo linasadikiwa kuwa na pochi iliyokuwa na fedha hizo.


Matrona alisema shahidi wa pili ambaye ni mlinzi wa duka hilo, Michael amedai kuwa msanii huyo alikataa kupekuliwa.

Alidai kuwa, msanii huyo alikataa kupekuliwa baada ya kumfuatilia nyendo zake tangu alipotoka katika duka hilo na kuingia katika duka la jirani kutafuta nywele za bandia' wiving'.

Michael alidai hayo jana katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, mbele ya Hakimu Matrona Luanda, ambapo shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Katika kesi hiyo, Isha (28) na Halima Shabani (26), wanadaiwa Aprili 20, mwaka huu, saa 12.45 jioni, mtaa wa Mafia na Jangwani, maeneo ya Kariakoo bila halali na kwa makusudi waliiba pochi ya mkononi iliyokuwa na sh. 758,000 kutoka dukani kwa Sara Peter, mali ya Veronica Taki.

Akitoa ushahidi wake, Michael alidai siku ya tukio akiwa nje ya duka kwa ajili ya kulinda mali za nje, waliingia hao wateja na walikaa ndani kwa takriban saa moja wakichambua 'mawigi'.

Michael alidai akiwa nje, hakujua kilichokuwa kikiendelea ndani na kwamba baada ya wateja hao kutoka alimuona muuza duka akitoka na kumuambia pochi yake imeibiwa.

Alidai muuza duka huyo alimueleza walioiba pochi hiyo ni wateja waliotoka mwisho (Isha na Halima), na hivyo aliamua kuwafuatilia na kuwakuta katika duka la pili.

Shahidi huyo, alidai alipowafuatilia dukani kwa mara ya kwanza aliwaeleza waende kuchukua wivingi walilokuwa wakilitafuta kwani duka linataka kufungwa.

Alidai aaliwafuata tena kwa mara ya pili ambapo walimjibu kwamba wafunge duka na watoke na hilo wigi nje. Hata hivyo, alidai Isha na wenzake hawakurudi katika hilo duka na kwenda katika gari lao na alipowaeleza juu ya upotevu wa pochi walishangaa na kudai wao si wezi.

Shahidi huyo alidai mama mwenye nyumba alipowafuata, Isha alikataa kupekuliwa na kuacha namba zake za simu kwa madai anawahi kipindi. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa Mei 22, mwaka huu.
 

Saturday, May 4, 2013

ISHA MASHAUZI ATINGA KIZIMBANI



MWIMBAJI mahiri wa nyimbo za taarab nchini, Isha Mashauzi na mwenzake, wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na shitaka la wiz wa fedha taslimu sh. 758, 200.
Isha na Halima Shabani (26) walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, mbele ya Hakimu Matrona Luanda.
Karani wa mahakama hiyo, Blanka Shayo alidai kuwa, washitakiwa walitenda kosa hilo Aprili 20 mwaka uu saa 12 jioni katika mtaa wa Mafia na Jangwani, wilayani Ilala.
Alidai kuwa, Isha na Halima waliiba pochi ya Veronica Taki, iliyokuwa na fedha taslimu sh. 758, 200 kutoka dukani kwa Sarah Peter, kMWIMBAJI mahiri wa nyimbo za taarab nchini, Isha Mashauzi na mwenzake, wamepandishwa kizimbani wakikabiliwa na shitaka la wiz wa fedha taslimu sh. 758, 200.
Isha na Halima Shabani (26) walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, mbele ya Hakimu Matrona Luanda.
Karani wa mahakama hiyo, Blanka Shayo alidai kuwa, washitakiwa walitenda kosa hilo Aprili 20 mwaka uu saa 12 jioni katika mtaa wa Mafia na Jangwani, wilayani Ilala.
Alidai kuwa, Isha na Halima waliiba pochi ya Veronica Taki, iliyokuwa na fedha taslimu sh. 758, 200 kutoka dukani kwa Sarah Peter, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, washitakiwa walikana shitaka hilo na walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Washitakiwa hao baada ya muda, walitolewa rumande kwa ajili ya kupatiwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kila mshitakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja watakaotia saini bondi ya sh. milioni 1.5. Kesi hiyo itatajwa tena Mei 14 mwaka huu.itendo ambacho ni kinyume cha sheria.
Hata hivyo, washitakiwa walikana shitaka hilo na walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Washitakiwa hao baada ya muda, walitolewa rumande kwa ajili ya kupatiwa dhamana baada ya kutimiza masharti.
Kila mshitakiwa alitakiwa awe na mdhamini mmoja watakaotia saini bondi ya sh. milioni 1.5. Kesi hiyo itatajwa tena Mei 14 mwaka huu.

Saturday, April 27, 2013

ISHA MASHAUZI 'AUZIWA' KESI YA WIZI


MKURUGENZI wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani ‘Mashauzi’ jana alionja adha ya umaarufu baada ya kusoteshwa kituo cha polisi cha Msimbazi huku kamera za waandishi maarufu zikimsubiri nje ya kituo hicho.
Isha alifikishwa kituoni hapo kwa kuhusishwa na upotevu wa shilingi laki saba uliotokea kwenye duka moja la Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa duka hilo la nywele, amemfikisha Isha na mwenzake aitwae Halima kituoni hapo akidai alipotelewa na kiasi hicho cha pesa huku msanii huyo akiwa ni wa mwisho kuingia dukani mwake.

Saluti5 ilifika kituoni hapo majira ya 5 za usiku na kukuta waandishi wengi wakimsubiri Isha atoke ili wapate picha, jambo ambalo walifanikiwa licha ya Isha kujitahidi kuwakwepa.
Inaaminika mmiliki wa duka hilo alipiga simu karibu kwa kila chombo cha habari ili waandishi wafike hapo akiamini kuwa jambo hilo litasaidia kumdhalilisha msanii huyo.

Akiongea na Saluti5 muda mfupi baada ya kutoka kituoni hapo, Isha alisema alifika dukani kwa dada huyo Jumamosi iliyopita lakini baada ya kukosa alichokifuata aliingia duka lingine na kuliacha gari lake jirani na duka hilo.
Wakati anarudi kwenye gari lake, wafanyakazi wawili wa duka hilo wakamfuta na kumwambia kuna upotevu wa pesa umetokea.

Isha anasema baada ya mjadala wa muda mrefu  akaawachia namba ya simu na kuwaambia iwapo bado watahitaji ufafanuzi zaidi wawasiliane.
Isha anasema: “Kuanzia Jumatatu alianza kunipigia simu za vitisho na kuniambia atanikomesha na kunidhalilisha.

“Vitisho vilipokithiri, Jumanne jioni nikaenda kituo cha Msimbazi kuripoti juu ya vitisho vyake, lakini kituoni wakaninyima ushirikiano wakaniambia niende Kinondoni ninakoishi.

“Nikawaambia nimekuja Msimbazi kwa vile biashara ya mtu anayenipa vitisho hivyo ipo Kariakoo, lakini bado walikataa kunihudumia.

“Nilirudi nyumbani nikipanga kuwa kesho yake niende kituo cha Oysterbay lakini leo (jana) nikapigiwa simu kutoka Msimbazi kuwa nifike kituoni hapo.

“Nikadhani labda sasa wameamua kunisikiliza, nilipofika kituoni hapo nikawekwa chini ya ulinzi kwa tuhuhuma za wizi wa shilingi laki 7.”

Baada ya kusota kwa masaa kadhaa Isha aliruhusiwa lakini akitakiwa kurudi tena kituoni hapo siku inayofuata (leo).

Watu kadhaa walifika kituoni hapo kumwekea dhamana Isha ambaye aligoma kabisa kuingizwa mahabusu.

Waliofika hapo akiwepo mtangazaji wa Times FM, Dida walifikia hata hatua ya kutaka kulipa pesa hizo lakini Isha alikataa kabisa jambo hilo lisifanyike akidai hii ni aina mpya ya utapeli.

“Haiwezekani duka ambalo lina wafanyakazi wawili na wateja wengi wanaoingia useme mtu fulani kakuibia.

“Kwanza mteja unakuwa nyuma ya kaunta yao na si rahi kujua pesa zilipo, utalivuka vipi hilo kaunta mpaka ufike kwenye pesa bila wahusika kukuona?

“Kwanini wasinikamate muda huo huo na kunipigia kelele za mwizi?” alihoji Isha.
Askari mmoja wa kituo hicho aliiambia Saluti5 kuwa malalamiko ya kesi hiyo yana mushkel na yamekaaa kiujanja ujanja ujanja.

Ameshangaa ni kwanini tukio la Jumamosi liachiwe hadi Jumatano, akashaangaa pia namna waandishi walivyotaarifiwa tukio hilo ndani ya muda mfupi.
IMEHAMISHWA KUTOKA SALUTI 5

Friday, April 19, 2013

SERIKALI ZANZIBAR ILIGHARAMIA MAZISHI YA BI KIDUDE



Na Othman Khamis Ame, OMPR
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeamua kugharamia mazishi ya Gwigi la Sanaa ndani ya ukanda wa Afrika ya Mashariki na mipaka yake Anti Fatma Binti Baraka { Maarufu Bi Kidule } aliyefariki dunia juzi mchana baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Hatua hiyo imekuja kufuatia mchango wake katika kuitangaza sanaa ya Zanzibar nje ya mipaka ya Tanzania hasa kwenye fani ya muziki wa Taarabu asilia na ile ngoma maarufu ya Unyago inayotumika katika sherehe za harusi.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akiifariji familia ya Marehemu Bi Kidude wakati wa matayarisho ya mazishi yake hapo Mtaani kwake Rahaleo nyuma ya Kituo cha ZBZ Redio, Rahaleo Mjini Zanzibar.
Balozi Seif akitoa ubani wa shilingi Milioni 2,000,000/- kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa familia ya marehemu alisema jamii na waswahili wote katika mwambao wa Afrika Mashariki wanafahamu mchango mkubwa wa Msanii Bi Kidude katika fani ya muziki wa taarabu.
Alisema Zanzibar imepata sifa kubwa katika Nyanja za Kimataifa kutokana na mchango wa wasanii kwa kueneza sanaa ya Taarabu iliyotoa fursa kwa baadhi ya watalii na wataalamu kuvitembelea Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameitaka Familia ya Msanii Bi Kidude kuwa na moyo wa subra katika kipindi hichi kigumu cha msiba na kuwaeleza kwamba msiba huo sio wao peke yao.
“ Kwa kweli sisi sote tunampenda sana Bi Fatma Binti Baraka { Bi Kidude }. Lakini tuelewe kwamba Mwenyezi muungu anampenda zaidi na ndio maana akamuhitaji Bi Kidude,“ alinasihi Balozi Seif.
Naye Mmoja wa wana Familia hiyo, Bwana Haji Ramadhan Suwed Buda kwa niaba ya Familia ya Marehemu Bi Kidude ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wake wa kuungana nao katika msiba huo.
Bwana Haji alisema hatua hiyo ya Serikali imeleta faraja kwao na kupunguza machungu ya msiba huo.
Msanii Gwiji wa sanaa ya Taarab asilia na ngoma ya Unyago Marehemu Bi Kidude aliyekadiriwa kufikia umri wa zaidi ya miaka 98, aliwahi kuolewa mara mbili, lakini hakupata Mtoto.
Mwenyezi Muungu ailaze roho ya marehemu Bi Kidude mahali pema.

MAZISHI YA BI KIDUDE PICHANI


Jeneza lenye mwili wa marehemu Bi Kidude likitolewa kwenye msikiti, ambako mwili wake uliswaliwa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Seif Sharrif Hamad akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Bi Kidude wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana Zanzibar.
Rais Jakaya Kikwete akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Fatuma Binti Baraka'Bi Kidude' wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana Zanzibar.
Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond' akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Bi Kidude
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Sheni akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Bi Kidude wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana Zanzibar.

Wednesday, April 17, 2013

WASEMAVYO WASANII KIFO CHA BI KIDUDE


BAADHI ya wasanii wa filamu na muziki nchini wameeleza kusikitishwa na kifo cha msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Fatuma Binti Baraka, maarufu zaidi kwa jina la Bi Kidude.
Wakizungumza na magazeti ya Burudani na Uhuru jana, wasanii hao walisema kifo cha msanii huyo mkongwe ni pigo kubwa katika tasnia ya taarab nchini.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilsoni Makubi alisema, kifo cha Bi Kidude ni pengo kubwa kwa wasanii kwa vile alikuwa akichukuliwa kuwa mfano wa kuigwa na wasanii.
Makubi alisema tasnia ya sanaa ilimtumia Bi Kidude katika sehemu mbili, moja katika muziki na nyingine katika filamu na kufanikisha kazi zao kuwa nzuri na za kuvutia.
Alisema msanii huyo alikuwa kiraka kwani kila alichoombwa kukifanya, alishiriki kikamilifu bila kuharibu kazi za wahusika na alijitolea kufanya kazi na wasanii wengi bila kujali aina ya kazi na umri wa wahusika.
Alisema pia kuwa, Bi Kidude alikuwa balozi wa wasanii katika nchi za nje kwa kuwa wengi waliifahamu Tanzania kupitia kazi zake na hivyo kuinufaisha kiutalii.
"Ukiangalia katika matamasha mengi yaliyokuwa yakifanyika Zanzibar kama vile ZIFF, watalii wengi walikuwa wakimfuata Bi Kidude," alisema Makubi.
Msanii nyota wa filamu nchini, Jacob Steven 'JB' alisema taarifa za kifo cha msanii huyo zilimshtua, lakini kwa vile ni kazi ya Mungu, haina makosa.
JB alisema wasanii wa Tanzania wanapaswa kujifunza mengi kupitia kwake ili kuuenzi mchango wake katika muziki wa taarab.
Mwanamuzi Judith Wambura, maarufu kwa jina la Lady JayDee, kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika: "Mungu ni mwema na mapenzi yake yatimizwe kwa kuwa msanii huyo ameweza kufanikisha mengi katika uhai wake na hasa kuwa mfano kwa wasanii wengi."
Jay Dee alisema atamkumbuka msanii huyo kupitia wimbo wake wa 'Muhogo wa Jang'ombe', ambao aliuimba kwa mara ya pili na kuwa moja ya nyimbo zilizompatia umaarufu.
"Ukitaka kujua kama Bi Kidude alikuwa kipenzi cha watu na alisaidia mafanikio ya wasanii wengi, angalia waliofanya naye kazi jinsi kazi zilivyopata mafanikio," alisema Jay Dee.
Mkurugenzi wa kikundi cha Jahazi, Mzee Yussuf alisema, amesikitishwa na kifo cha mkongwe huyo na kumuombea mapumziko mema.
Alisema katika kumuenzi msanii huyo, atatayarisha wimbo mmoja
utakaoelezea wasifu wake na kazi zake.
Mkurugenzi wa kikundi cha taarab cha Wanawake cha Zanzibar, Maryam Mohammed Hamdan alisema, kifo cha Bi Kidude ni pigo zima kwa taifa kwa vile alikuwa kipenzi cha wengi.
Uongozi wa Tamasha la Sauti za Busara umesema, ilikuwa vigumu kwao kuamini taarifa za msiba wa msanii huyo kutokana na kuzushiwa kifo mara kwa mara.

BI KIDUDE HATUNAYE, KUZIKWA LEO Z'BAR


Na Aboud Mahmoud, Zanzibar
MSANII mkongwe wa fani ya muziki wa taarab nchini, Fatuma Binti Baraka, maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia.
Bi Kidude alifariki dunia leo saa 6:45 mchana nyumbani kwa mtoto wa ndugu yake, maeneo ya Bububu, Zanzibar baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya msiba huo kuhamishiwa nyumbani kwake maeneo ya Rahaleo, mmoja wa wajukuu wa marehemu, Omar Ameir alisema, marehemu Bi Kidude alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa idi na sukari.
"Bi Kidude alikuwa akiugua kwa muda mrefu na kutibiwa katika hospitali mbalimbali hapa nchini. Mara ya mwisho alitibiwa katika hospitali ya KMKM,"alisema.
Kwa mujibu wa Ameir, mazishi ya Bi Kidude yanatarajiwa kufanyika kesho mchana kijiji kwake Kitumba, Wilaya ya Kati mkoa wa Kusini Unguja.
Hali ya afya ya Bi Kidude ilianza kuzorota kuanzia mwishoni mwa mwaka jana na kusababisha alazwe katika hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam.
Wakati alipolazwa kwenye hospitali hiyo, watu wengi walikuwa wakipishana kwenda kumsalimia, wengine wakitoka nje ya nchi.
Jambo moja kubwa, ambalo Bi Kidude alikuwa akililaani vikali wakati huo ni taarifa za kuzushiwa kufariki dunia.
“Watu wamenizushia kufa na wewe hukuja kuniona, ulifikiri nimekufa? Mi mzima, si unaniona, cheki,”alisema Bi Kidude huku akiuvuta
mkono wa mwandishi wa makala hii kwa nguvu, akiuminya ‘kibaunsa’ kuonyesha nguvu za misuli yake, kwamba yeye yuko mzima.
Bi Kidude alilazwa kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya sukari, ambayo alikuwa akiugua kwa kwa muda mrefu, lakini yalimzidia kutokana na kukiuka taratibu za vyakula.
“Kweli nilikuwa naumwa, ngozi yote ilivuka hii, nilikonda sana, ila sasa Alhamdulillah mi mzima, naweza kuondoka,”alisema.
Muda wote, ambao Bi Kidude amekuwa akiugua, alikuwa akiuguzwa na watoto wa ndugu zake. Hakubahatika kuzaa.
Ndugu wote watatu, ambao ni wadogo zake Bi Kidude, walishafariki dunia. Alikuwa anakula matunda ya watoto wa ndugu zake hao, ambao ndio waliokuwa wakimlea.
Baada ya kutolewa katika hospitali hiyo, Bi Kidude hakuruhusiwa kufanyakazi yoyote ya saa. Alitakuwa kupumzika. Pia alipigwa marufuku na madaktari kuvuta sigara.
Bi Kidude alikuwa gwiji wa muziki katika Bara la Afrika, katika fani ya mwambao, ambayo hujulikana kwa jina la taarabu. Muziki huu ambao ni mchanganyiko wa vionjo kutoka nchi za Kiarabu na Kiafrika, umetikisa sana katika mwambao wa Afrika Mashariki, yaani Zanzibar, Mombasa, Lamu na kwingineko.
Marehemu Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimarigo, Zanzibar katika familia ya watoto saba (7). Baba yake, Mzee Baraka alikuwa ni mfanyabiashara wa nazi.
Wakati wote wa uhao wake, hakuwa akifahamu tarehe halisi aliyozaliwa, isipokuwa alichojua ni kwamba, alizaliwa wakati rupia ikitumika kama fedha na kwamba ilikuwa kabla ya Vita Kuu ya Kwanza ya Ulaya.
Wataalamu wa mahesabu baada ya kupata taarifa hizo, walimpigia hesabu na kumkabidhi miaka yake kwamba ni zaidi ya miaka 100.
Bi Kidude alianza uimbaji tangu alipokuwa na umri wa miaka 10 na alijifunza kutoka kwa msanii mkongwe na aliyetamba enzi hizo, Sitti Binti Saad.
Wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali walikuwa wakifika Zanzibar kwenda kumuona Sitti na kwa vile alikuwa karibu na Bi Kidude, yeye ndiye aliyewapeleka nyumbani kwake na kupata nafasi ya kumsikia akiwaimbia.
Alipokuwa na umri wa miaka 13, kwa mara ya kwanza alitoroka nyumbani kwao Zanzibar na kukimbilia Tanzania Bara. Alifanya hivyo
baada ya kulazimishwa kuolewa.
Hata hivyo, alipokuwa kigoli wa kutosha kuolewa, aliolewa japokuwa ndoa hiyo  haikudumu kutokana na manyanyaso aliyokuwa akiyapata. Hivyo aliamua kukimbilia kaskazini mwa Misri ikiwa ni katika miaka ya 1930.
Akiwa Misri, aling'ara katika fani yake ya uimbaji na uchezaji ngoma. Lakini ilipofika miaka ya 1940, aliamua kurudi nyumbani Zanzibar ambako aliendelea na shughuli zake za uimbaji.
Enzi za uhai wake, Bi Kidude hakuwa akitegemea kazi moja tu ya kuimba. Alikuwa akifanya biashara zingine kama vile kuuza 'wanja' na 'hina', ambavyo alivitengeneza mwenyewe.
Mkongwe huyo pia alikuwa mtaalamu wa matibabu kwa dawa za mitishamba. Zaidi ya hayo, alikuwa mwalimu mzuri wa 'Unyago' na aliwahi kuanzisha chuo chake. Aliwahi kutamba kuwa,
katika wanafunzi wake wote, hakuna aliyepata talaka kutoka kwa mumewe.
Marehemu Bi Kidude amewahi kutembelea nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Oman, Ufaransa, Hispania, Ufini, Ujerumani na Uingereza. Pia amewahi kupata tuzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi (ZIFF) 1999.
Mwaka jana, mkongwe huyo alipata tuzo ya WOMAX. Miongoni mwa nyimbo alizowahi kuimba na kumpatia umaarufu ni Muhogo wa Jang'ombe.
Hakuwahi kupata elimu nyingine zaidi ya Quraan.

BURIANI MANJU HAJI MOHAMED


HATIMAYE safari ya miaka 55 ya msanii nguli na mkongwe wa fani ya muziki wa taarab nchini, Haji Mohamed Omar ilikoma Jumatatu iliyopita baada ya kufariki dunia kutokana na ugonjwa wa sukari.
Marehemu Haji, ambaye alikuwa mkurugenzi wa kundi la East African Melody, alifariki dunia saa nne asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, ambako alipelekwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kutojisikia vizuri.
Mazishi ya Haji yalifanyika juzi Zanzibar na kuhudhuriwa na mamia ya watu, wakiwemo wasanii mbalimbali wa muziki huo.
Kifo cha Haji ni pengo kubwa katika muziki wa taarab, hasa ile ya kisasa. Licha ya kuwa mmoja wa waanzilishi wa kundi la East African Melody, alikuwa mtunzi na mwimbaji mzuri wa muziki huo.
Marehemu Haji ni uzao wa mwasisi wa taarab visiwani Zanzibar, hayati Sitti binti Saad na amewahi kupanga muziki katika nyimbo nyingi za East African Melody.
Haji amekuwa msanii wa pili wa kundi la East African Melody kupoteza maisha katika kipindi cha miezi minne iliyopita. Januari mwaka huu, msanii mwingine nyota wa kikundi hicho, Lamania Shaaban naye alipoteza maisha kutokana na ugonjwa wa sukari.
Kundi la East African Melody lilianzishwa 1990 nchini Oman. Miongoni mwa waasisi wa kundi hilo ni Haji, Lamania, Peter Dawo, Ashraf Mohamed, Mlamali Adam na Mahmoud Al-Alawi.
Waimbaji wa mwanzo wa kundi hilo ni pamoja na Zuhura Shaaban, Rukia Ramadhani, Sihaba Muchacho, Khadija Yussuf, Khadija Kopa na Othman Soud.
Marehemu Haji alianza kupata umaarufu baada ya kuibuka na kibao chake cha kwanza katika kundi hilo kinachojulikana kwa jina la Majamboz na Mavituz.
Kwa kawaida, marehemu Haji alikuwa mpole, lakini alikuwa mcheshi kwa mtu alizomzoea. Ni kiongozi aliyeweza kuwafanya wasanii wa East African waishi kama ndugu kwa kusaidiana kimaisha.
Wakati kundi hilo lilipohamishia maskani yake katika Jiji la Dar es Salaam likitokea Zanzibar, Haji ndiye aliyewashawishi viongozi wenzake kununua nyumba maeneo ya Magomeni Mapipa, Dar es Salaam na kuwa makao makuu yao.
Katika upande mmoja wa nyumba hiyo, waliishi wasanii wa kike na upande mwingine waliishi wasanii wa kiume. Nyumba hiyo pia ilitumika kwa ajili ya mazoezi ya kundi hilo.
Akizungumza na mwandishi wa makala hii nyumbani kwake mtaa wa Livingstone, Kariakoo, Dar es Salaam 2002, Haji alisema waliamua kuhamishia maskani yao Tanzania Bara kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mashabiki.
Miongoni mwa nyimbo za East African Melody, ambazo marehemu Haji alishiriki kuzitayarisha ni pamoja na Kinyago cha Mpapure, Bure yako, Pata leo, Hatusemani hatuchekani, Halo yako, Kama wewe hakuna, Penzi, Kipo kinachonivutia.
Marehemu Haji pia ndiye mtunzi wa nyimbo za Taxi Bubu, Shecky lesi, Sorry kwa huyu siye, Mnikome na Joho la Mungu.
Mmoja wa viongozi wa kundi hilo, Mlamali amekiri kuwa, kifo cha Haji ni pengo jingine kubwa, ambalo itakuwa vigumu kuzibika baada ya kumpoteza msanii wao mwingine Lamania.
"Ni kweli vifo vya Lamania na Haji ni pengo kubwa kwa East African Melody, lakini hatuna budi kusonga mbele,"alisema.
Kwa mujibu wa Mlamali, kundi hilo kwa sasa litakuwa chini ya Peter Dawo, ambaye atarithi cheo cha ukurugenzi, akisaidia na Ashraf.
Marehemu Haji alisoma elimu ya msingi katika shule ya Vikokotoni na kuhitimu darasa la sita 1976. Alisoma masomo ya sekondari katika shule ya Forodhani na kumaliza 1980.
Alianza kujifunza muziki katika vikundi vidogo vya muziki huo vya Zanzibar kabla ya kujiunga na kikundi kikongwe cha Ikhwan Safaa kabla ya kutua East African Melody.

BREAKING NEEWSSSS. BI KIDUDE AFARIKI DUNIA



Habari tulizozipata hivi punde zimeeleza kuwa, msanii mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Baraka Mohamed, maarufu kwa jina la Bi Kidude amefariki dunia.

Kwa mujibu wa habari hizo, Bi Kidude amefariki dunia saa sita mchana nyumbani kwake Zanzibar.

Habari zaidi kuhusu kifo cha mkongwe huyo wa taarab tutawaletea baada ya muda mfupi ujao.

Monday, April 15, 2013

BREAKING NEWSSSS, HAJI MOHAMED WA EAST AFRICAN MELODY AFARIKI DUNIA

 Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa, msanii mkongwe na muziki wa taraab wa  kikundi cha East African Melody,  Haji Mohamed 'Kijukuu cha Siti Bint Saad, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa habari hizo, Haji amefariki dunia leo saa nne asubuhi  wakati akipelekwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam baada ya kuzidiwa na presha.

Taarifa zimeeleza kuwa, marehemu Haji  alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya sukari na presha kwa muda mrefu.

Kifo cha Haji kimetokea miezi michache baada ya msanii mwingine wa kundi hilo, Lamania Shaaban kufariki dunia kwa ugonjwa wa kisukari.

Mwili wa marehemu Haji ulitarajiwa kusafirishwa leo mchana kwa boti ya Azam Marine kupelekwa Zanzibar kwa ajili ya mazishi.

Mkurugenzi wa East African Melody, Hashim Salum amesema leo kuwa, alipata nafasi ya kuzungumza na marehemu asubuhi na kumwambia kwamba
alikuwa anakwenda hospitali kuonana na daktari wake.

Marehemu Haji ameacha mke na watoto watatu.
Mungu ailaze roho yake mahali pema.

Friday, March 29, 2013

SHAKILA: MWASISI WA TAARAB ALIYESIMAMA JUKWAANI KWA ZAIDI YA MIAKA 40


“'Macho yanacheka, moyo unaliaaa, macho yanacheka aeeh, moyo unalia, nikimkumbuka wangu my dear ''
Hayo ni baadhi ya maneno yaliyo katika wimbo aliouimba Bi Shakila alipokuwa na Bendi ya JKT miaka 1980 -1990, ambao ulijizolea umaarufu mkubwa ndani ya Tanzania na Afrika Mashariki.

Mkongwe huyo aliolewa mwaka 1960 alipokuwa na umri wa miaka 11 na mwanamume ambaye alizaa naye mtoto mmoja.

Shakila Said Khamis maarufu kwa jina la Bi Shakira  ni mmoja wa waasisi wa muziki wa Taarabu nchini, ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Waimbaji wa Taarabu Tanzania.

Katika mahojiano na Starehe, Bi Shakila alieleza kuwa alianza kuimba taarabu sambamba na marehemu Saada Binti Saad, mwaka 1960 baada tu ya kuolewa na baadaye moja kwa moja alijiunga katika Bendi ya JKT aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 40.

"Nilianza muziki mwaka 1960 kabla ya Uhuru na nimekuwa huko kwa miaka mingi. Kabla ya kuanza muziki, nilimkuta marehemu Saada Binti Saad, Bi Kidude yeye nilimkuta akiwa tayari amejiunga na ngoma za Unyago, alikuwa bibi yangu na mtu wa karibu sana na mimi wakati huo nilikuwa na miaka sita.”

Hayo ni baadhi ya maelezo ya awali Bi Shakila katika mahojiano na Starehe nyumbani kwake Charambe, Dar es Salaam, kabla ya mfululizo ufuatao wa maswali na majibu na mwandishi wa makala haya.

Mwandishi: Hali yako kiuchumi kwa sasa ikoje?

Bi Shakila: Sina pesa, kiwango ninachokipata kama kiinua mgongo hakinitoshi kabisa. Nalipwa Sh80,000 kwa mwezi na NSSF, matumizi yangu kwa siku ni zaidi ya Sh15,000 kwa siku. Nilistaafu mwaka 2009, lakini mpaka sasa huwa naendelea na kazi yangu pale JKT mara chache na kama tukifanya shoo huwa napewa nauli Sh3000 inayonisaidia kunirudisha nyumbani. Kwa sasa hali yangu ni mbaya kiuchumi.

Mwandishi: Katika kipindi chote cha kazi yako hukuweza kujiwekea vitega uchumi, kama ndivyo sababu ni zipi?

Bi Shakila: Zamani muziki ulikuwa kama starehe, tulilipwa ujira mdogo na hata kukiwa na shoo tulipata ujira mdogo. Kwa sasa muziki ni ajira, tena kubwa kuliko ofisini, lakini umri umeshaenda sana na sisi wakongwe tunatamani haya yangekuwepo hapo nyuma, hii ndiyo sababu ya mimi kushindwa kuweka vitega uchumi.

Mwandishi: Unadhani Serikali inaweza kukusaidia?

Bi Shakila: Kabisa, sisi wakongwe hatuthaminiwi na tunatupwa jalalani, lakini watoto wadogo wavuta unga ndiyo wanasaidiwa, Msanii Ray C alienda mwenyewe kuvuta unga akijua kabisa ni kinyume cha sheria, lakini Serikali imemsaidia, kwa nini na sisi tusiangaliwe? Sisi ni dhahabu, wapo kina Mzee Gurumo, Small, Bi Kidude hivi sasa ni wagonjwa na wanahitaji msaada ila hawasaidiwi mpaka tufe ndiyo waje kutuzika?

Mwandishi: Pole! Wewe huamka saa ngapi na nini majukumu yako ya kutwa nzima?

Bi Shakila: Naamka saa 11 alfajiri kwa ajili ya kuanza kuandaa unga wangu wa vitumbua na maandazi, baada ya hapo naanza kupika. Alhamdulilahi, nina wateja kidogo wanaoniungisha. Saa4 asubuhi namaliza, napumzika kidogo na kuanza kuanza kutengeneza visheti hadi saa 12 jioni. Naoga, napumzika na wanangu tunazungumza mawili matatu kisha naenda kulala hadi kesho tena. Kama ninakwenda mazoezi JKT, basi siku hiyo ratiba yangu huvurugika kidogo. Biashara ya vitumbua nimeifanya kwa miongo minne sasa.

Mwandishi: Kwa kulinganisha na wakati wenu, unadhani taarabu ya sasa inakua?

Bi Shakila: Taarabu kwa sasa hakuna. Kwa sasa kuna rusha roho, mipasho, kiduku na  khanga moja. Vitu hivi vimevamia na kuiharibu taarabu yetu. Zamani taarabu ilikuwa na ustaarabu na waimbaji tuliimba kwa staha na maneno yalikuwa ya kuburudisha na kusifia kitu fulani si sasa hivi. Hii wanaita Morden Taarabu mimi siikubali kabisa.

Mwandishi: Maisha yako ya ndoa yalikuwaje?

Bi Shakila: Niliozwa nilipokuwa na miaka 11. Mume aliyenioa kwa ndoa aliniacha mwaka mmoja baadaye kwa kuwa tulitofautiana kwa mengi. Aliniacha nikiwa na mtoto mmoja mchanga, hapo ndipo nilipoanza balaa hilo. Niliolewa tena na mume mwingine huyu niliishi naye miaka 18 na kuzaa naye watoto watano, mwaka 1975 alifariki, iliniuma sana nikakaa eda.
Baadaye niliolewa na mume mwingine, huyu nikazaa naye watoto watano na baadaye tuliachana. Nikaolewa tena kwa mara ya nne, nikazaa watoto wawili, nilipokuwa na mimba ya huyu mtoto wa mwisho mwaka 1993, mume akaniacha. Mwanangu wa mwisho Shani nilimzaa Ijumaa ya tarehe 27 Machi 1993. Tangu hapo niliwachukia wanaume na sijataka kuolewa tena mpaka leo.

Mwandishi: Waimbaji wa muziki wa taarabu waume kwa wanawake huoa sana au kuolewa na kuachika, tatizo ni nini?

Bi Shakila: Sijui, kwa kweli mimi siyo kwamba nilikuwa nikiacha wanaume, hapana ila walikuwa wakiniacha wao. Kwa upande wangu nahisi ilitokana na kuwa mwanamuziki na wakati huo muziki ulichukuliwa kama uhuni. Lakini huenda kuna sababu nyingine ambazo mimi sizijui.

Mwandishi: Tangu kustaafu umeshafikiria kufanya kazi ya muziki ukiwa mwenyewe?

Bi Shakila: Ndiyo, tangu nimestaafu nilianza kufanya kazi nikiwa na mwanangu na mpaka sasa nipo mwishoni kumalizia albamu yangu ya Mama na Mwana itakayokuwa na nyimbo nane. Kati ya hizo tano zimekamilika ikiwamo ya Mama na Mwana.

MAKALA HII NI KWA HISANI YA GAZETI LA MWANANCHI.

Thursday, March 7, 2013

ALLY STAR AVUNJA UKIMYA



BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mwimbaji taarab mkongwe nchini, Ally Hemed Star ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Mvuvi Kinda.

Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Ally alisema amekirekodi kibao hicho kwa mtindo wa zing zong, nje ya kundi lake la Tanzania One Theatre (TOT-Plus).

Ally alisema kibao hicho kitakuwemo kwenye albamu yake binafsi, anayotarajia kuizindua hivi karibuni, ambayo ameirekodi kwa mtindo huo.

Alisema anaushukuru uongozi wa TOT Plus kwa kumruhusu kurekodi nyimbo zake binafsi kwa lengo la kujiongezea mapato.

Mkongwe huyo wa taaab alisema, muziki huo kwa sasa unalipa, tofauti na miaka ya nyumba ndio sababu si rahisi kwa msanii kutunga wimbo na kumpa msanii mwingine auimbe.

"Enzi zetu, msanii akitunga wimbo, alikuwa anafikiria ampe nani aimbe na atampatia mwimbaji, ambaye anaendana na wimbo huo kutokana na maudhui yake,"alisema.

"Lakini siku hizi, mtu akitunga wimbo mzuri, hataka kumpa mwingine kwa hofu ya kumpatia sifa na umaarufu,"aliongeza.

Ally alisema kutokana na muziki wa taarab kuwa na malipo mazuri hivi sasa, kila msanii anataka kutoka kivyake kwa lengo la kujiongezea mapato.

Ally alianza kupata umaarufu katika taarab wakati alipokuwa akiimbia kikundi cha Bima Modern Taarab kabla ya kutua Muungano Cultural Troupe na baadaye TOT Plus.

SIJAITOSA MASHAUZI CLASSIC-THABITI


MSANII nyota wa muziki wa taarab nchini, Thabit Abdul amesema uamuzi wake wa kujiunga na kikundi cha taarab cha Five Stars hauna maana kwamba amekitosa kikundi chake cha Mashauzi Classic.
Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Thabiti alisema amejiunga na Five Stars kwa makubaliano maalumu na kwamba bado ataendelea kuitumikia Mashauzi Classic.
Thabit, ambaye ni mmoja wa wapiga vinanda mahiri nchini alisema, uongozi wa Five Stars umemruhusu kufanya maonyesho na kikundi cha Mashauzi Classis kila atakapokuwa na nafasi.
Alisema kwa sasa yeye si msanii wa kupiga muziki jukwaani kwa muda mrefu kwa sababu kazi yake kubwa ni kutunga, kutengeneza muziki na kupiga ala.
"Katika kikundi cha Mashauzi Classic, sina kawaida ya kupiga nyimbo nyingi stejini. Naweza kupiga wimbo mmoja ama mbili tu kwa sababu wapo vijana wanaofanya kazi hiyo,"alisema.
Alipoulizwa atawezaje kuvitumikia vikundi vyote viwili iwapo vitakuwa na maonyesho kwa wakati mmoja, Thabit alisema kikundi chake cha kazini ni Five Stars.
"Inapotokea hivyo, lazima nikitumikie kikundi cha Five Stars, ambacho nina mkataba nacho,"alisisitiza.
Thabit ni mmoja wa wakurugenzi wa Mashauzi Classic, kinachoongozwa na mwimbaji machachari wa kike, Isha Mashauzi.
Hata hivyo, msanii huyo wiki iliyopita alitangaza kujiunga na Five Stars, ambacho kimesukwa upya baada ya kupata uongozi mpya. Wasanii wengine waliojiunga na kikundi hicho ni Mwanahawa Ally, Sabah Salum, Hammer Q, Maua Tego na Mosi Suleiman.

Tuesday, February 19, 2013

FIVE STARS MODERN TAARAB CHASUKWA UPYA



KIKUNDI cha taarab cha Five Stars kimewanyakua nyota wapya wa muziki huo kutoka katika vikundi mbalimbali kwa lengo la kujiimarisha.

Miongoni mwa wasanii hao wapya ni pamoja na waimbaji wakongwe, Mwanahawa Ally, Sabah Salum, Maua Tego, Mosi Suleiman na mpiga kinanda Thabiti Abdul.

Mbali na kuajiri nyota hao, kundi hilo pia limeupiga chini uongozi wote wa zamani na kuweka viongozi wapya.

Kwa sasa, kundi hilo ambalo lilitamba vilivyo mwaka juzi kabla ya wasanii wake 14 kufariki dunia kwa ajali ya gari, lipo chini ya mkurugenzi, Maalim Sharrif Mambo maarufu kwa jina la Shacks.

Wasanii wa zamani wa kundi hilo waliofariki dunia kwa ajali ni Issa Kijoti, Sheba Juma, Tizzo Mgunda, Omary Hashim, Omary Haji, Hajji Mzania, Nassoro Madenge, Husna Mapande, Hamisi Omary, Maimuna Makuka, Hassan Ngeleza, Ramadhani Maheza na Ramadhani Mohamed.

Kiongozi wa kundi hilo, Ally J aliwaambia waandisi wa habari mjini Dar es Salaam jana kuwa, wameamua kulisuka upya kundi hilo ili kuhimili ushindani wa taarab uliopo sasa.

Wasanii wengine wapya waliojiunga na kundi hilo ni Jumanne Ulaya, Yussuf Tego, Mariam Mohamed, Mariam Omary na Hammer Q.

Jay alisema wasanii hao wameingia mkataba wa miaka miwili na Five Stars kila mmoja na kundi hilo linatarajiwa kuingia kambini wakati wowote kwa ajili ya kuandaa albamu mpya.

Kwa upande wake, Shacks alisema kundi lake halina uhasama na kundi lolote na kwamba ujio wao umelenga kuongeza ushindani katika muziki wa taarab na kusaka fedha kwa kutoa vitu vya uhakika.

Alisema tayari wamefanya makubaliano na Jahazi Modern Taarab ili kutochukuliana wasanii. Katika makubaliano hayo, viongozi wa makundi hayo mawili hawatapokea msanii kutoka kundi lingine.

Mbali na kuingia mkataba huo, Shacks alisema makundi hayo mawili yamekubaliana kushirikiana katika kuendeleza muziki wa taarab.

Friday, February 15, 2013

MASHAUZI CLASSIC WAKIWA KAZINI

AISHA Othman wa kundi la Mashauzi Classic akikamua jukwaani wakati wa onyesho lililofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
ISHA Mashauzi akiwajibika jukwaani wakati wa onyesho hilo

SHABIKI huyu akiwa amepagawa kutokana na utamu wa sauti ya Isha Mashauzi

SAIDA Mashauzi akituzwa na mashabiki wakati wa onyesho hilo

SAIDA Mashauzi akiimba kwa hisia kali, akilalamikia penzi

MASHAUZI APATA KITAMBULISHO CHA UTAIFA

 
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha na msanii wa muziki wa Taarab, Aisha Mashauzi, baada ya kumkabidhi kitambulisho cha Taifa, wakati wa uzinduzi wa zoezi la kukabidhi vitambulisho vya Taifa jana mjini Zanzibar. Mashauzi ni miongoni mwa wananchi kutoka Tanzania Bara waliopewa vitambulisho vyao katika hafla ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,kwa mara ya kwanza kwa Upande wa Zanzibar,hafla iliyofanyika katika viwanja vya Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje ya Mji wa Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.