KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, December 6, 2016

TMK TAARAB KUTAMBULISHWA RASMI KWA MASHABIKI DESEMBA 17



NA VICTOR MKUMBO

TANZANIA ni miongoni mwa nchi za Ukanda wa Pwani, ambazo zina bendi nyingi za muziki wa taarabu.

Muziki wa taarabu umekuwa ukipandachati kila kukicha na wasanii mbalimbali wanaibuka na kufanya vyema.

Hata hivyo,kuna aadhi ya bendi zimekuwa zikianzishwa mara kwa mara na kufanya vizuri, lakini zingine zikifa kutokana na sababu mbalimbali.

Pia,uongozi mbovu unachangia wasanii wengi kuhama bendi moja hadi nyingine kutokana na maslahi duni, tofauti na zamani, ambapo walifanyakazi kwa moyo hata kama hawapati kiwango cha fedha cha kuridhisha.

Kwa sasa, kuna ushindani mkubwa ndani ya muziki huo huku wasanii wakongwe wakitamani kutoka kwenye bendi kubwa na kuhamia katika bendi zisizokuwa na majina makubwa ili kufuata neema.

Bendi mpya ya taarabu ya TMK Modern, imeanzishwa kwa mara ya kwanza waka huu, ikiwa imesheheni wasanii wakongwe, ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuipa mafanikio kutokana na umahiri wao.

Wasanii, wakongwe waliojiunga na bendi hiyo, wametoka katika bendi za muziki wataarabu ambazo zinatamba kwa sasa kwa ajili ya kuongeza upinzani ndani ya tasnia hiyo.

Kutokana na jinsi uongozi waTMK Modern Taarab, kujipanga vyema, huenda ikawa moja ya bendi ambazo zitatikisa kwenye muziki huo na watu wanasubiri kwa hamu kuona vitu vipya.

Bendi hiyo inaongozwa na Mkurugenzi, Said Fella, mbaye ni mmoja wa watu waliodumu kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu.

Wasanii ambao wapo chini ya Fella wamekuwa akifanikiwa zaidi kila kukicha na kufanya matamasha ndani na nje ya nchi.

Fella anamiliki kituo cha wasanii cha kubwa na Wanawe, ambapo ndani yake kuna wasanii wa kila sanaa.

Kituo hicho kimetambulika kwa kuwatoa wasanii wachanga na kufanya vyema kwenye tasnia ya muziki, tofauti na jinsi ilivyokuwa inatarajiwa na wengi.

Wapo wasanii ambao wametokea kwa Fella na kwa sasa wanafanya vizuri na nyimbo zao haziishi kusikilizwa na kutazamwa na mashabiki wa muziki katika ukanda wa AfrikaMashariki.

Kundi la TMK Modern Taarab, linaundwa na wasanii nguli kina Mwanahawa Ally, FatmaMcharuko, Aisha Vuvuzela, Maua Tego na OmaryTego.

Wasanii waliotoka Mkubwa na Wanawe ni Amina Mnyalu, Jeza Adam, Hassan Saleh na Ibrahim Said.

Wapiga ala ni Mussa Mipango, Father Mauji, Chid Boy na Babu Ally ambao wamejikitika katika upande wa kupiga gita na kinanda.

Akizungumzia kundi hilo hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji, OmaryTego, alisema wameanzisha bendi hiyo mwaka huu ili kuhakikisha wanaleta mapinduzi katika muziki wa taarab nchini.

Alisema kwa kiasi kikubwa wamejipanga, hivyo wana imani kubwa yakuufikisha mbali muziki wa taarab.

Alisema bendi hiyo inaundwa na wasanii wakongwe waliopitia katikabendi mbalimbali za muziki wa aarab ili kuhakikisha wanasimama vyema.

Alisema kuna changamoto mbalimbali wasanii wanaounda kundi hilo,
ambazo wamepitia awali na hivyo kuamua kuunda kundi la pamoja na kurudi upya katika muziki huo.

“Wasanii wanaounda kundi la TMK Modern Taarab, wametokea atika bendi mbalimbali, ili kuhakikisha tunafikia malengo kwani pia wamepitia kwenye changamoto nyingi hadi kufika hapa walipo sasa,” amesema.

Anasema kuwa adi sasa wameshakamilisha kurekodi jumla ya nyimbo saba ambazo zitakuwepo kwenye albamu zao mpya zitakazotoka mwakani.

Amesema kuwa baadhi ya nyimbo zimeshaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na kufanya vizuri.

Nyimbo zilizoanza kusikika ni pamoja na Figisufigisu zimekwisha, mtunzi akiwa Tego, Sina pupa Mungu atanipa, iliyoimbwa na Manahawa, Kibaya kina mwenyewe ya Aisha Vuvuzela na Ndoa, iliyoimbwa na Jeza Adam.
 “Nyimbo ambazo zimeshakamilika zimetungwa kwa ustadi mkubwa na hivyo msikilizaji hatachoka kupata burudani safi, ikiwa ni pamoja na ujumbe uliopo,” amesema.

Mkurugenzi huyo anasema kuwa bado wapo katika mikakati ya kuboresha kundi lao ili kuhakikisha linaimarika zaidi.

Amesema kuwa apo wasanii wakubwa kutoka kwenye bendi kongwe, ambao wanatarajiwa kujiunga nao hivi karibuni.

“Tumejipanga vyema kuhakikisha tunafanya mapinduzi kwenye muziki wa taarab kwani pia bado tupo kwenye mikakati ya kuimarisha kundi letu. Kuna baadhi ya wasanii ambao watajiunga na sisi hivi karibuni na wanatoka kwenye bendi kongwe,” amesema.

Ameongeza uwa wanatarajia kufanya uzinduzi wa kuitambulisha rasmi bendi hiyo Desemba 17, mwaka huu, katika onyesho la kwanza litakalofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live.

Amesema uwa uzinduzi huo unatarajiwa kuwa wa aina yake kutokana na maandalizi ya muda mrefu waliyoyafanya.

Katika uzinduzi huo, watasindikizwa na wasanii mbalimbali, wakiwemo  Amani Temba na Said Chege, Dullah Makabila, Madada sita kutoka Mkubwa na Wanawe na kundi zima la The African Stars ‘TwangaPepeta’.

Baada ya uzinduzi huo, wataendelea kufanya maandaliziyaalbamu zao mbili, ambazo zitatoka kwa mpigo.

No comments:

Post a Comment