KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Monday, October 31, 2016

KUNDI JIYA LA TAARAB LA TMK LAIBOMOA JAHAZI, COAST MODERN TAARAB


Ule usemi unaosemwa na baadhi ya wadau wa taarab ya kuwa "Jahazi Modern Taarab bila ya Mzee Yussuf linasuasua" unaonekana kama unakubalika kwa asilimia fulani baada ya bendi hiyo kupoteza waimbaji muhimu pamoja na wapiga vinanda.

Majina ya Fatma Nyoro, Chidi Boy, Moh'd Mauji, Mussa Mipango, Kichupa kwa sasa hayatosikika kwenye maonesho ya Jahazi.

Pia kuna tetesi kuwa Khadija Yussuf ameenda Wakaliwao kwa Thabit Abdul.

Bendi ya TMK pia imeibomoa Coast Modern Taarab kwa kumpa shavu Omary Teggo na dada yake.
Pia Bi Mwanahawa Ali (JEMBE GUMU) ametilishiwa saini katika bendi hiyo huku akipewa wimbo wa "SINA PUPA MUNGU ATANIPA".

Thursday, October 20, 2016

ISHA MASHAUZI, LEYLA RASHID NANI ZAIDI KUONYESHANA KAZI KESHOKUTWA DAR
NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”.  Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.

Onyesho hilo linasosubiriwa kwa hamu kubwa litafanyika Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Saalam.

Bendi mbili kubwa za taarab, Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic ndiyo zitakazosindikiza mpambano wa mahasimu hao wawili.

“Sura Surambi” ni moja ya nyimbo ambazo piga ua lazima iwe kweye ratiba ya Isha Mashauzi wakati iwe isiwe Leyla naye lazima aidumbukize ngoma yake ya “Nina Moyo Sio Jiwe” katika orodha ya nyimbo atakazotumbuiza.

Tangu onyesho hilo litangazwe, waimbaji hao wameingia kwenye vita vikubwa vya maneno ambapo kila mmoja amejinasibu kuibuka na ushindi.