KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Wednesday, September 24, 2014

HIVI NDIVYO VIBAO VIPYA VINAVYOTAMBA MITAANI HIVI SASA


                                                      Hammer Q - Kibakuli

                                          Sina Makuu - Ashura Machupa - G5 Modern Taarab...

                                         Hassan Voucher Ft Hasna - Sindano na Golkeeper

                                        Mtu Mzima hovyooo- Wakali wao Modern Taradance

ABDUL MISAMBANO AFUFUKA, AJA NA MPYA ISEMAYO 'SI MIE NI MOYO'
Msanii mkongwe katika muziki wa miondoko ya taarabu nchini,  Abdul Misambano, ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la 'Si mie ni moyo'.

Hii ni mara ya kwanza kwa Misambano kutoa kibao kipya baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa.

Msanii huyo aliyewahi kung'ara katika kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema hivi karibuni kuwa, alifanikiwa kurekodi kibao hicho hivi karibuni baada ya kukifanyia mazoezi kwa wiki
kadhaa.

Misambano amesema katika kibao hicho, kinanda kimepigwa kwa umaridadi mkubwa na mkali wa kupapasa ala hiyo, Omary Kisira.

Kwa wanaomkumbuka Misambano, alijipatia umaarufu mkubwa kupitia kibao chake cha Asu kilichotamba miaka ya 1990.

ISHA MASHAUZI AACHIA RHUMBA NZITO, AMEIMBA PEKE YAKE MWANZO MWISHONYOTA wa miondoko ya taarab, Isha Ramadhani 'Mashauzi' amekuja kivingine
ambapo ameachia rhumba kali la miondoko ya muziki wa dansi.
Ngoma hiyo inakwenda kwa jina la 'Nimlaumu Nani'.

Ni wimbo wa dakika tano uliorekodiwa katika studio ya Soft Records
chini ya producer Pitchou Meshaa.

Sauti zote utakazozisikia katika wimbo huu, zimewekwa na Isha Mashauzi mwenyenye – ameimba
peke yake mwanzo mwisho.