KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Friday, June 7, 2013

KHADIJA KOPA ALIVYOUPOKEA MSIBA WA MUMEWEBaadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege
 msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania, Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa
 ndege wa mpanda baada ya  kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri  kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimisho ya
 siku ya Mazingira Duniani kitaifa  yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto)akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo Bi Khadija Kopa alikua kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.

2 comments:

  1. May the Lord God grant you all peace through the Lord Jesus Christ and may there be comfort to all at this time, especially to the widow, dear Lady!

    ReplyDelete