KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, September 17, 2013

MWIMBAJI AHMED MGENI WA ZANZIBAR STARS AFARIKI DUNIAMWIMBAJI  wa kikundi cha taarabu cha Zanzibar Stars, Ahmed Mgeni, amefariki dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mmoja wa ndugu wa marehemu, alisema Mgeni alifariki jana saa kumi na mbili asubuhi katika hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.

Alisema marehemu alikuwa akisumbuliwa na kichwa na alianza kuugua tangu mwezi wa nne mwaka huu lakini baadae alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Alisema, hali ya marehemu ilibadilika ghafla juzi na kukimbizwa hosipitali kabla ya mauti kumfika na kusema alizikwa jana katika makaburi ya Mwanakwerekwe, Zanzibar.

Akiwa na kundi la Zanzibar Stars, marehemu aliwahi kutamba na nyimbo mbalimbali na mapema mwaka huu alianzisha kundi lake la muziki wa taarabu lililoitwa Nia Njema.

No comments:

Post a Comment