KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, January 13, 2015

ONYESHO LA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk (kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Pili Seif Iddi (kulia) akiwa na Waziri wa Kilimo na Maliasili, Dk. Sira Ubwa Mamboya
 Baadhi ya wananchi na mashabiki wa Taarab waliohudhuria katika hafla ya Taarab hiyo ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Mtumwa Mbarouk akiimba wimbo wa "Mpewa hapokonyeki" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Waimbaji wa  Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Asha Alli  na Khamis Nyange, wakiimba wimbo wa Miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, uliotungwa na Profesa Gogo
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Saada Mohammed akiimba wimbo unaosema  "kweli nnae" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja [Picha na Ikulu]

No comments:

Post a Comment