KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Monday, January 5, 2015

ISHA MASHAUZI KUREKODI WIMBO WA MCHIRIKU


Baada ya kutesa na wimbo wake wa rhumba “Nimlaumu Nani” Isha Mashauzi sasa anajiandaa kuachia ‘single’ nyingine, safari hii ikiwa katika miondoko ya mchiriku.

Akiongea na Saluti5, Isha alisema wimbo huo utakwenda wa jina la “Ado Ado” na utarekodiwa wiki hii kabla ya kauchiwa redioni mwishoni mwa mwezi huu.

“Ni ngoma ya dakika nne ambayo sina shaka kuwa itakimbiza ile mbaya,” alisema Isha.

Isha amesema baada ya kauchia mchiriku, ataachia wimbo mwingine ambao uko katika miondoko ya mutwashi, wimbo ambao umepewa jina la “Usisahau”.

“Lengo langu ni kutoa albam yenye jumla ya nyimbo sita ambayo itakuwa nje kabisa ya miondoko ya taarab, alisema Isha na kuongeza: “Nataka kudhihirisha kuwa nina uwezo wa kuimba aina yoyote ya muziki.”

No comments:

Post a Comment