KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, February 3, 2015

WAKALI WAO MODERN TARADANSI WAJA NA VIBAO VIWILI VIPYA, MISAMBANO ASHUSHA MOJA KALIKUNDI jipya la muziki wa taarab la Wakali Wao Modern Taradansi, limeibuka na vibao vingine viwili vipya.

Vibao hivyo, ambavyo tayari vimeshaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini ni Kumbe ndio tabia yake na Jasho la mnyonge hulipwa na Mola.

Kibao cha Kumbe ndio tabia yako kimeimbwa na mwanadada Nasra Shaaban wakati kibao cha Jasho la mnyonge hulipwa na Mola kimeimbwa na kiongozi wa kundi hilo Thabit Abdul.

Akizungumza na mtandao huu wiki hii, Thabit alisema ujio wa vibao hivyo viwili ni maandalizi ya ujio wa albamu yao mpya, inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Alisema tayari wameshakamilisha vibao viwili na kwamba vingine vitatu bado vipo jikoni na vinatarajiwa kupakuliwa hivi karibuni.

Thabit alisema kama ilivyo kawaida, wamepiga vibao hivyo kwa miondoko ya taarabu ya kisasa kwa lengo la kuwavutia zaidi mashabiki.

Wakati huo huo, mkali wa miondoko ya taarab, Abdul Misambano naye ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Sio mie ni moyo.

No comments:

Post a Comment