Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Saada Mohammed akiimba wimbo unaosema "kweli nnae" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja [Picha na Ikulu]
Tuesday, January 13, 2015
ONYESHO LA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Saada Mohammed akiimba wimbo unaosema "kweli nnae" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja [Picha na Ikulu]
Monday, January 5, 2015
OGOPA KOPA ILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI DAR LIVE
ISHA MASHAUZI KUREKODI WIMBO WA MCHIRIKU
Baada ya kutesa na wimbo wake wa rhumba “Nimlaumu Nani” Isha Mashauzi sasa anajiandaa kuachia ‘single’ nyingine, safari hii ikiwa katika miondoko ya mchiriku.
Akiongea na Saluti5, Isha alisema wimbo huo utakwenda wa jina la “Ado Ado” na utarekodiwa wiki hii kabla ya kauchiwa redioni mwishoni mwa mwezi huu.
“Ni ngoma ya dakika nne ambayo sina shaka kuwa itakimbiza ile mbaya,” alisema Isha.
Isha amesema baada ya kauchia mchiriku, ataachia wimbo mwingine ambao uko katika miondoko ya mutwashi, wimbo ambao umepewa jina la “Usisahau”.
“Lengo langu ni kutoa albam yenye jumla ya nyimbo sita ambayo itakuwa nje kabisa ya miondoko ya taarab, alisema Isha na kuongeza: “Nataka kudhihirisha kuwa nina uwezo wa kuimba aina yoyote ya muziki.”
Subscribe to:
Posts (Atom)