KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Sunday, July 20, 2014

MASHAUZI CLASSIC KUZINDUA ALBAMU MPYA IDDI MOSI



KIKUNDI cha Taarab cha Mashauzi Classic, chini ya uongozi wake Isha Mashauzi, siku ya Idd Mosi kitafanya onyesho la uzinduzi wa albamu yake mpya ya 'Asiyekujua hakuthamini.'

Onyesho hilo litakaloanza saa tatu usiku, limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Buzuruga Plaza na kiingilio kitakuwa sh. 10,000 kwa mtu mmoja.

Katika onyesho hilo, kutakuwepo  wasanii machachari wenye sauti za kuvutia kama vile Isha Mashauzi (mkurugenzi), Hashim Said,  Thania Msomali, Saida Ramadhani na Zubeidah Andunje.

No comments:

Post a Comment