Wednesday, June 12, 2013
MASHAUZI AFUTIWA MASHITAKA
Na Sylvia Sebastian,DSJ
MWIMBAJI nyota wa taarabu nchini, Isha Ramadhani, maarufu kwa jina la Isha Mashauzi, ameachiwa huru na Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, Dar es Salaam kutokana na upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yake bila kuacha shaka.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Matrona Luanda baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wake na Mashauzi na mshitakiwa mwenzake, Halima Shaaban kutoa utetezi wao.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Matrona alisema kuwa mahakama hiyo inawaachia huru Mashauzi na Halima, ambao walikuwa wakikabiliwa na shitaka la wizi wa mkoba uliokuwa na fedha taslim sh. 758,200 mali ya muuza duka Sarah Peter.
Alisema kuwa upande wa Jamhuri umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa bila ya kuacha shaka yoyote.
Mashauzi na mwenzake, walikuwa wakidaiwa kutenda kosa hilo, Aprili 20, mwaka huu, mtaa wa Mafia na Jangwani, walipoingia dukani kwa ajili ya kununua nywele bandia.
Wakati wa usikilizwaji wa shauri hilo, Sarah ambaye ni muuza duka la Veronica Taki, alidai kuwa washitakiwa waliingia dukani siku hiyo ya tukio saa moja kasoro usiku, ambapo walifanikiwa kuchukua pochi iliyokuwa na fedha hizo ambazo ni za mauzo ya siku.
Monday, June 10, 2013
RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA KHADIJA KOPA
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiifariji familia na ndugu jamaa wa msanii maarufu wa taarabu na mjumbe wa Halmashauri kuu taifa CCM Hadija Koppa kufuatia kifo cha mumwewe Jaffari Ali Yusuf kilichotokea wiki iliyopita na kuzikwa jijini Dar es Salaam.Wapili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Ahmed Kipozi na kulia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa CCM Bwana Ridhwani Kikwete(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Koppa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumwewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Msanii wa taarabu Hadija Koppa nyumbani kwake mjini Bagamoyo jana kufuatia kifo cha Mumwewe Marehemu Jaffari Ali Yusuf aliyefariki na kuzikwa wiki iliyopita.
Friday, June 7, 2013
KHADIJA KOPA ALIVYOUPOKEA MSIBA WA MUMEWE
Baadhi ya viongozi na wananchi wa mkoa wa Rukwa na Mpanda wakimsindikiza kupanda ndege
msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania, Khadija Omar kopa kwenye uwanja wa
ndege wa mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo alfajiri kutokana na ugonjwa, Bi Khadija Kopa alikua akitokea kwenye Maadhimisho ya
siku ya Mazingira Duniani kitaifa yaliyoadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Mkuu wa mkoa Rukwa Eng. Stalla Manyanya (kushoto)akimfariji msanii wa taarab na malkia wa mipasho Tanzania,Khadija omar Kopa alipokua kwenye chumba maalum cha kupumzikia wageni kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya kupewa taarifa ya kufiwa na mumewe Jafari Ali Yussuf aliyefariki Dunia leo Bi Khadija Kopa alikua kwenye maadhimisho ya siku ya mazingira Duniani kitaifa
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
yaliyoaadhimishwa Namanyere Mkoani Rukwa jana.
Thursday, June 6, 2013
BREAKING NEWSSSS...KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE
Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.
Subscribe to:
Posts (Atom)