Isha Mashauzi, kiongozi na mwimbaji wa Mashauzi Classic ameshika mkia
MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Mwanahawa Ally ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka mwimbaji bora wa muziki huo.
Mwanahawa, ambaye amewahi kuimbia vikundi mbalimbali vya taarab nchini, aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga waimbaji wengine wanne.
Shindano hilo liliandaliwa na blogu ya Rusha Roho, ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuandika habari na makala za wasanii wa muziki wa taarabu.
Katika shindano hilo, Mwanahawa alipata kura sita, ambazo zimepigwa na wasomaji wa blogu hiyo, zikiwa sawa na asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
Mwimbaji mwingine mkongwe wa muziki huo, Khadija Kopa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura tano, ambazo ni sawa na asilimia 41.
Khadija Yussuf alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura nne, ambazo ni sawa na asilimia 33, akifuatiwa na Leila Rashid, aliyepata kura tatu, ambazo ni sawa na asilimia 25. Isha Mashauzi alishika mkia kwa kupata kura mbili, sawa na asilimia 16.
Blogu ya Rusha Roho inawashukuru wale wote walioshiriki kupiga kura za kumtafuta msanii bora wa taarab kati ya wasanii hao watatu.
KHADIJA KOPA 5 (41%)
LEILA RASHID 3 (25%)
ISHA MASHAUZI 2 (16%)
KHADIJA YUSUF 4 (33%)
MWANAHAWA ALLY 6 (50%)
No comments:
Post a Comment