Monday, April 21, 2014
ASIA IDAROUS: MUZIKI WA MWAMBAO ASILIA UNA MGUSO WAKE
Na Andrew Chale
MWANAMITINDO mkongwe na mdau wa muziki wa mwambao asilia, Asia Idarous Khamsin, amesema muziki huo una mguso wake hivyo jamii inatakiwa kuupokea na kuuenzi.Asia ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, alisema hayo usiku wa April 19, wakati wa onesho maalumu la Usiku wa Mwambao Asilia, ambalo pia lilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU, sasa AU), Dk. Salim Ahmed Salim, aliyekuwa mgeni rasmi akiungana na wadau wengine katika kuenzi muziki huo ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam.Asia alisema katika kuenzi muziki huo ni pamoja na kuwakumbuka wanamuziki wakongwe walioufikisha hapo ulipo.“Baadhi ya nyimbo za mwambao asilia unapozisikiliza zinagusa moja kwa moja, na ujumbe wake hufika kwa haraka,” alisema Asia.Katika onesho hilo, Asia alidhihirisha umahiri wake na kuimba kibao cha ‘Raha ya Moyo Wangu’.Bendi za Dar Modern Taarab na Nadd Ikhwan (Malindi), zilikonga nyoyo wadau wa miondoko hiyo waliofurika ndani ya ukumbi huo huku wakipata pia wasaha wa kupita kwenye zuria jekundu na kupiga picha za ukumbusho, ambapo awali kwenye miondoko ya taarab hapa nchini haikuwa na utamaduni huo wa red carpert.Onesho hilo lilidhaminiwa na Times FM, Fabak Fashions na www.nakshi255.com na wengine wengi wakiwemo mashughuli blog, Michuzi blog, Vijimambo blog simu tv na wengine wengi
Tuesday, April 1, 2014
SUNGURA MJANJA WA MASHAUZI ATOA KITU KIPYA
MWIMBAJI chipukizi wa tarab anayeinukia vizuri nchini, Saida Ramadhani ‘Sungura Mjanja’, ameibuka na wimbo mpya uitwao Ropokeni Yanayowahusu.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam, mwimbaji huyo wa kundi la Mashauzi amesema wimbo huo ametungiwa na dada yake, Isha Ramadhani.
“Dada Isha katunga, mimi nimerekodi na umekwishakamilika, ni wimbo mzuri sana, naamini utapendwa ukitoka. Na utazidi kunipandisha matawi ya juu,”alisema Saida.
Saida ameingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za Kili mwaka huu kupitia wimbo wa Asiyekujua Hakuthamini, ambao ameshirikiana na dada yake, Isha ulioingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa Taarab.
ISHA MASHAUZI AIBUKA NA SURA SIYO ROHO
MWANAMUZIKI na kiongozi wa kundi la taarab la Mashauzi Classic, Isha Mashauzi, ametoa nyimbo mpya mbili, ambazo muda si mrefu zitaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Redio nchini.
Akizungumza na BIN ZUBEIRY jioni hii katika hoteli ya Double Tree, Masaki, Dar es Salaam wakati wa semina ya wanamuziki waliongia kwenye tuzo za Kili 2014, Isha au Jike la Simba amesema kwamba nyimbo zote ni nzuri.
Amezitaja nyimbo hizo kuwa ni Sura Siyo Roho na Mapenzi Hayana Dhamana, ambazo zote ametunga yeye mwenyewe.
“Kama kawaida, wapenzi na mashabiki wangu na mashabiki wa Mashauzi Classic kwa ujumla, wajiandae kwa kazi mpya, tutaanza na audio (sauti) baadaye itafuatia na kwenye video pia,”alisema Isha.
FATIHYA AKIWA NDANI YA MAONYESHO YA BIASHARA COCO BEACH
MFANYABIASHARA Fatihya Masoud (kushoto) akifurahia jambo wakati akimueleza mteja, Farida Shekigenda, bei ya mabegi alipotembelea banda lake juzi kwenye maonyesho ya biashara ya Kariakoo yanayofanyika kwenye ufukwe wa Coco Beach kwa udhamini wa Kampuni ya Simu ya Tigo.
MFANYABIASHARA Fatihya Masoud (kushoto) akimueleza mteja, Farida Shekigenda, bei ya mabegi alipotembelea banda lake juzi kwenye maonyesho ya biashara ya Kariakoo yanayofanyika kwenye ufukwe wa Coco Beach kwa udhamini wa Kampuni ya Simu ya Tigo.
MFANYABIASHARA Fatihya Masoud akifurahia vipodozi vyake wakati wa maonyesho hayo
Subscribe to:
Posts (Atom)