Tuesday, December 20, 2016
SIJAWAHI KUOMBA TALAKA KWA MUME WANGU-LEYLA
MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab nchini, Leyla Rashid amesema kamwe hajawahi kuomba talaka kutoka kwa mumewe, Mzee Yusuph.
Aidha, Leyla amesema anajisikia upweke kuendelea kuimba nyimbo za muziki huo bila kuwa karibu na Mzee.
Leyla alisema hayo hivi karibuni, baada ya kudaiwa kuwepo na shinikizo la kumtaka aachane na muziki huo na kuungana na mumewe, ambaye kwa sasa ameacha kuimba taarab na kuwa alhaji.
Hivi karibuni, dada wa Mzee Yusuph, Khadija Yusuph, alikaririwa akisema kuwa, Layla anafanya makosa kuendelea kuimba taarab wakati mumewe ameachana na muziki huo.
Khadija alisema kwa mujibu wa sheria za dini ya kiislamu, mke anapaswa kufuata maelekezo ya mumewe iwapo amemtaka kuachana na fani ambayo yeye ameshaiacha.
Akijibu tuhuma hizo, Leyla alisema ni kweli amewahi kugombana na mumewe mara kadhaa, lakini kamwe hakuwahi kuomba talaka.
Pia, alisema sio kweli kwamba Mzee aliwahi kumtishia kwamba atampa talaka iwapo hataacha kuendelea kujihusisha na muziki huo.
"Hajaniambia acha, isipokuwa mimi mwenyewe najihisi kupungukiwa na kitu fulani.Nilizoea tunakuwa pamoja stejini, lakini sasa hayupo tena,"alisema Leyla.
Mwanamama huyo alisema hadi sasa hajaamua nini la kufanya, bali anamuachia Mungu na kusisitiza kuwa, ni kawaida kwa binadamu kutokosa la kusema, lakini hababaishwi na maneno yao.
"Kama mtu anasema, mwache aseme, mdomo ni mali yake," alisema mwanamama huyo mwenye watoto wawili na kusisitiza kuwa, muda wa kuachana na muziki huo ukifika, atafanya hivyo.
Leyla alisema mumewe hadi sasa hajaonyesha shaka yoyote kwake kwa uamuzi wake wa kuendelea na muziki huo, zaidi ya kumtia moyo na kufuatilia maendeleo yake kila anaposafiri mikoani kwa maonyesho mbalimbali.
TMK MODERN TAARAB YAZINDULIWA KWA KISHINDO
KIKUNDI kipya cha taarab cha TMK Modern, mwishoni mwa wiki kilifanya onyesho kabambe la uzinduzi, lililofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mashabiki lukuki.
Katika onyesho hilo, kundi hilo lilisindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta, Madada sita na mwimbaji nyota wa muziki huo, Leila Rashid kutoka Jahazi.
Wakiongozwa na waimbaji nyota na wakongwe, Mwanahawa Ali, Omar Tego na Maua Tego, kundi hilo liliwafanya mashabiki wafurike kwa wingi stejini kucheza muda wote wa onyesho.
Wakati huo huo, uongozi wa kundi jipya la muziki wa taarab nchini, 'Yah TMK Modern Taarab', umewataka wapenzi wa muziki huo, kuipokea bendi yao ambayo inaanza rasmi maonyesho yake ya katika kumbi mbalimbali hapa nchini.
Mkurugenzi wa kundi hilo, Said Fella amesema baada ya kufanya utambulisho wa kundi hilo mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Dar Live, sasa wanaanza rasmi maonyesho katika kumbi mbalimbali za burudani hapa nchini.
Fella alisema kundi hilo litaanza onyesho lake la kwanza Desemba 23, mwaka huu, kwenye ukumbi wa CCM Kigamboni, wakati siku ya mkesha wa Krismas watakuwa kwenye ukumbi wa Mpo Africa, ulioko
Tandika.
Alisema Desemba 25, kundi hilo litakuwa ndani ya ukumbi wa Lekam ulioko Buguruni na Desemba 26, litakuwa kwenye ukumbi wa Lanch Time, Mazense.
Fella alisema kuwa kundi hilo limejipanga kutoa burudani ya aina yake na kudhihirisha kuwa, kwa sasa ndilo moto wa kuotea mbali.
"Lengo letu ni kutoa burudani, tumejipanga kutoa burudani ya aina yake, wanamuziki wapo vizuri na kila mtu anajisikia kufanya kazi yake vizuri kabisa," alisema Fella.
Kundi hilo linaundwa na wasanii mbalimbali nguli, akiwepo Mwanahawa Ali, Fatma Mcharuko, Aisha Vuvuzela, Omar Tego, Maua Tego na wapiga vyombo kina Mohamed Mauji, Mussa Mipango, Chid Boy (kinanda) na Babu Ally Kichupa.
Tuesday, December 13, 2016
ISHA MASHAUZI KUFUNGA NA KUFUNGUA MWAKA NA "KISS ME"
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa taarabu hapa nchini Aisha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi (pichani) anataraji kuachia kibao kipya cha kufunga na kufungua mwaka kitachokwenda kwa jina la "Kiss Me".
Akizungumza na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo Isha Msahauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari.
“Hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu. Hivyo mashabiki wangu wapendwa wajue kuwa nyimbo hiyo ambayo ipo katika viwango vya hali ya juu itakonga nyoyo zao", amesema Isha Mashauzi, akiongezea kuwa imefanywa katika studio za Sophia Records zilizopo kinondoni”
Ameongeza: "Waliniona nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hiki kibao ambacho watafurahi wenyewe...."
Akizungumza na Globu ya Jamii jijini Dar es salaam leo Isha Msahauzi amesema kuwa amekuwa kimya kwa kipindi kirefu hivyo kibao hicho kitaweza kuwarudisha mashabiki wake katika mstari.
“Hii ni zawadi ya kufunga na kufungua mwaka kwa mashabiki wangu. Hivyo mashabiki wangu wapendwa wajue kuwa nyimbo hiyo ambayo ipo katika viwango vya hali ya juu itakonga nyoyo zao", amesema Isha Mashauzi, akiongezea kuwa imefanywa katika studio za Sophia Records zilizopo kinondoni”
Ameongeza: "Waliniona nimekuwa kimya katika taarabu sasa nimerudi tena na hiki kibao ambacho watafurahi wenyewe...."
Tuesday, December 6, 2016
TMK TAARAB KUTAMBULISHWA RASMI KWA MASHABIKI DESEMBA 17
NA VICTOR MKUMBO
TANZANIA ni miongoni mwa nchi za Ukanda wa Pwani, ambazo zina bendi nyingi za muziki wa taarabu.
Muziki wa taarabu umekuwa ukipandachati kila kukicha na wasanii mbalimbali wanaibuka na kufanya vyema.
Hata hivyo,kuna aadhi ya bendi zimekuwa zikianzishwa mara kwa mara na kufanya vizuri, lakini zingine zikifa kutokana na sababu mbalimbali.
Pia,uongozi mbovu unachangia wasanii wengi kuhama bendi moja hadi nyingine kutokana na maslahi duni, tofauti na zamani, ambapo walifanyakazi kwa moyo hata kama hawapati kiwango cha fedha cha kuridhisha.
Kwa sasa, kuna ushindani mkubwa ndani ya muziki huo huku wasanii wakongwe wakitamani kutoka kwenye bendi kubwa na kuhamia katika bendi zisizokuwa na majina makubwa ili kufuata neema.
Bendi mpya ya taarabu ya TMK Modern, imeanzishwa kwa mara ya kwanza waka huu, ikiwa imesheheni wasanii wakongwe, ambao kwa namna moja au nyingine wanaweza kuipa mafanikio kutokana na umahiri wao.
Wasanii, wakongwe waliojiunga na bendi hiyo, wametoka katika bendi za muziki wataarabu ambazo zinatamba kwa sasa kwa ajili ya kuongeza upinzani ndani ya tasnia hiyo.
Kutokana na jinsi uongozi waTMK Modern Taarab, kujipanga vyema, huenda ikawa moja ya bendi ambazo zitatikisa kwenye muziki huo na watu wanasubiri kwa hamu kuona vitu vipya.
Bendi hiyo inaongozwa na Mkurugenzi, Said Fella, mbaye ni mmoja wa watu waliodumu kwenye tasnia ya muziki kwa muda mrefu.
Wasanii ambao wapo chini ya Fella wamekuwa akifanikiwa zaidi kila kukicha na kufanya matamasha ndani na nje ya nchi.
Fella anamiliki kituo cha wasanii cha kubwa na Wanawe, ambapo ndani yake kuna wasanii wa kila sanaa.
Kituo hicho kimetambulika kwa kuwatoa wasanii wachanga na kufanya vyema kwenye tasnia ya muziki, tofauti na jinsi ilivyokuwa inatarajiwa na wengi.
Wapo wasanii ambao wametokea kwa Fella na kwa sasa wanafanya vizuri na nyimbo zao haziishi kusikilizwa na kutazamwa na mashabiki wa muziki katika ukanda wa AfrikaMashariki.
Kundi la TMK Modern Taarab, linaundwa na wasanii nguli kina Mwanahawa Ally, FatmaMcharuko, Aisha Vuvuzela, Maua Tego na OmaryTego.
Wasanii waliotoka Mkubwa na Wanawe ni Amina Mnyalu, Jeza Adam, Hassan Saleh na Ibrahim Said.
Wapiga ala ni Mussa Mipango, Father Mauji, Chid Boy na Babu Ally ambao wamejikitika katika upande wa kupiga gita na kinanda.
Akizungumzia kundi hilo hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji, OmaryTego, alisema wameanzisha bendi hiyo mwaka huu ili kuhakikisha wanaleta mapinduzi katika muziki wa taarab nchini.
Alisema kwa kiasi kikubwa wamejipanga, hivyo wana imani kubwa yakuufikisha mbali muziki wa taarab.
Alisema bendi hiyo inaundwa na wasanii wakongwe waliopitia katikabendi mbalimbali za muziki wa aarab ili kuhakikisha wanasimama vyema.
Alisema kuna changamoto mbalimbali wasanii wanaounda kundi hilo,
ambazo wamepitia awali na hivyo kuamua kuunda kundi la pamoja na kurudi upya katika muziki huo.
“Wasanii wanaounda kundi la TMK Modern Taarab, wametokea atika bendi mbalimbali, ili kuhakikisha tunafikia malengo kwani pia wamepitia kwenye changamoto nyingi hadi kufika hapa walipo sasa,” amesema.
Anasema kuwa adi sasa wameshakamilisha kurekodi jumla ya nyimbo saba ambazo zitakuwepo kwenye albamu zao mpya zitakazotoka mwakani.
Amesema kuwa baadhi ya nyimbo zimeshaanza kusikika katika vituo mbalimbali vya redio na kufanya vizuri.
Nyimbo zilizoanza kusikika ni pamoja na Figisufigisu zimekwisha, mtunzi akiwa Tego, Sina pupa Mungu atanipa, iliyoimbwa na Manahawa, Kibaya kina mwenyewe ya Aisha Vuvuzela na Ndoa, iliyoimbwa na Jeza Adam.
“Nyimbo ambazo zimeshakamilika zimetungwa kwa ustadi mkubwa na hivyo msikilizaji hatachoka kupata burudani safi, ikiwa ni pamoja na ujumbe uliopo,” amesema.
Mkurugenzi huyo anasema kuwa bado wapo katika mikakati ya kuboresha kundi lao ili kuhakikisha linaimarika zaidi.
Amesema kuwa apo wasanii wakubwa kutoka kwenye bendi kongwe, ambao wanatarajiwa kujiunga nao hivi karibuni.
“Tumejipanga vyema kuhakikisha tunafanya mapinduzi kwenye muziki wa taarab kwani pia bado tupo kwenye mikakati ya kuimarisha kundi letu. Kuna baadhi ya wasanii ambao watajiunga na sisi hivi karibuni na wanatoka kwenye bendi kongwe,” amesema.
Ameongeza uwa wanatarajia kufanya uzinduzi wa kuitambulisha rasmi bendi hiyo Desemba 17, mwaka huu, katika onyesho la kwanza litakalofanyika kwenye ukumbi wa Dar Live.
Amesema uwa uzinduzi huo unatarajiwa kuwa wa aina yake kutokana na maandalizi ya muda mrefu waliyoyafanya.
Katika uzinduzi huo, watasindikizwa na wasanii mbalimbali, wakiwemo Amani Temba na Said Chege, Dullah Makabila, Madada sita kutoka Mkubwa na Wanawe na kundi zima la The African Stars ‘TwangaPepeta’.
Baada ya uzinduzi huo, wataendelea kufanya maandaliziyaalbamu zao mbili, ambazo zitatoka kwa mpigo.
Subscribe to:
Posts (Atom)