Sunday, January 24, 2016
ISHA MASHAUZI SASA HAKAMATIKI
Mwimbaji bora wa kike wa taarab Isha Mashauzi, amezidi kudhihirisha kuwa yuko vizuri hata nje ya taarab baada ya kuachia ngoma yake mpya “JIAMINI” iliyoko katika miondoko ya zouk rumba.
Unaambiwa ngoma hiyo iliyofanywa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitchou Mechant, imetiwa mkono na mkali wa kinanda Fred Manzaka kutoka Mashujaa Band na mchawi wa bass Dekanto wa Akudo Impact huku solo gitaa likikung’utwa na Pitchou ambaye pia anaitumikia Akudo Impact.
Sauti zote utakazozikia kwenye wimbo huu wa dakika nne, ni za kwake Isha Mashauzi.
Hii inakuwa ngoma ya nne ya Isha Mashauzi nje ya taarab, baada ya “Nimlamu Nani”, “Nimpe Nani” na “Usisahau”
ISHA AWACHENGUA MASHABIKI WA TAARAB MWANZA, ATINGA STEJINI NA VIWALO VYA KILEO
HAIKUWA rahisi kuamini, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mwimbaji nyota wa kikundi cha taarab cha Mashauzi Classic, Isha Mashauzi, hivi karibuni aliwaacha hoi mashabiki wake mjini Mwanza baada ya kutinga stejini akiwa na viwalo vya kileo.
Uvaaji huo wa Isha ulikuwa tofauti na mavazi anayovaa awapo stejini, ambapo ni kawaida yake kuvaa magauni marefu ya kumeremeta kama ilivyo kwa waimbaji wengi wa taarab nchini.
Lakini siku hiyo Isha alivalia trucksuit nyeusi, raba na kofia nyeupe kichwani, mavazi yaliyomtoa vilivyo na kumfanya aonekane kama mwanamke kutoka majuu.
Isha alitinga na mavazi hayo stejini wakati wa onyesho la Baba na Mwana, kati yake na Mzee Yussuf lililofanyika kwenye ukumbi wa Villa Park mjini Mwanza.
Katika raundi ya kwanza ya onyesho hilo, Isha alivaa gauni la kawaida, kabla ya kubadili mwonekano raundi ya pili kwa kuvaa full trucksuit nyeusi na kuufanya ukumbi ulipuke mayowe ya kumshangilia.
CHANZO CHA HABARI: BLOGU YA ISHA MASHAUZI
Subscribe to:
Posts (Atom)