KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Sunday, October 12, 2014

MWANAHAWA ALLY AMBWAGA KHADIJA KOPA KATIKA NANI MKALI WA RUSHA ROHO


 Mwanahawa Ally, mwimbaji mkongwe  ameshika nafasi ya kwanza
 Khadija Kopa, mwimbaji wa TOT ameshika nafasi ya pili
 Khadija Yussuf, mwimbaji wa Jahazi ameshika nafasi ya tatu
LEILA Rashid, mwimbaji wa Jahazi ameshika nafasi ya nne
Isha Mashauzi, kiongozi na mwimbaji wa Mashauzi Classic ameshika mkia

MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Mwanahawa Ally ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka mwimbaji bora wa muziki huo.

Mwanahawa, ambaye amewahi kuimbia vikundi mbalimbali vya taarab nchini, aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga waimbaji wengine wanne.

Shindano hilo liliandaliwa na blogu ya Rusha Roho, ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuandika habari na  makala za wasanii wa muziki wa taarabu.

Katika shindano hilo, Mwanahawa alipata kura sita, ambazo zimepigwa na wasomaji wa blogu hiyo, zikiwa sawa na asilimia 50 ya kura zilizopigwa.

Mwimbaji mwingine mkongwe wa muziki huo, Khadija Kopa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura tano, ambazo ni sawa na asilimia 41.

Khadija Yussuf alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura nne, ambazo ni sawa na asilimia 33, akifuatiwa na Leila Rashid, aliyepata kura tatu, ambazo ni sawa na asilimia 25. Isha Mashauzi alishika mkia kwa kupata kura mbili, sawa na asilimia 16.

Blogu ya Rusha Roho inawashukuru wale wote walioshiriki kupiga kura za kumtafuta msanii bora wa taarab kati ya wasanii hao watatu.
  KHADIJA KOPA   5 (41%)
  LEILA RASHID   3 (25%)
  ISHA MASHAUZI   2 (16%)
  KHADIJA YUSUF   4 (33%)
  MWANAHAWA ALLY   6 (50%)

Wednesday, October 1, 2014

MBILI MPYA ZA ISHA MASHAUZI USIPIME






MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab na kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhani, ameibuka na kibao kingine kipya kinachokwenda kwa jina la Mapenzi hayana dalali.

Kibao hicho ni mwendelezo wa nyimbo mpya za Isha, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Nimlaumu nani, ambacho amekiimba kwa miondoko ya rhumba, akiimba sauti zote.

HII NI NGOMA MPYA YA AZIA MZINGA WA MASHAUZI CLASSIC



'Wema Hauozi Ubaya Haulipizwi' - Asia Mzinga ndani ya Mashauzi Classic