Tuesday, February 3, 2015
WAKALI WAO MODERN TARADANSI WAJA NA VIBAO VIWILI VIPYA, MISAMBANO ASHUSHA MOJA KALI
KUNDI jipya la muziki wa taarab la Wakali Wao Modern Taradansi, limeibuka na vibao vingine viwili vipya.
Vibao hivyo, ambavyo tayari vimeshaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini ni Kumbe ndio tabia yake na Jasho la mnyonge hulipwa na Mola.
Kibao cha Kumbe ndio tabia yako kimeimbwa na mwanadada Nasra Shaaban wakati kibao cha Jasho la mnyonge hulipwa na Mola kimeimbwa na kiongozi wa kundi hilo Thabit Abdul.
Akizungumza na mtandao huu wiki hii, Thabit alisema ujio wa vibao hivyo viwili ni maandalizi ya ujio wa albamu yao mpya, inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.
Alisema tayari wameshakamilisha vibao viwili na kwamba vingine vitatu bado vipo jikoni na vinatarajiwa kupakuliwa hivi karibuni.
Thabit alisema kama ilivyo kawaida, wamepiga vibao hivyo kwa miondoko ya taarabu ya kisasa kwa lengo la kuwavutia zaidi mashabiki.
Wakati huo huo, mkali wa miondoko ya taarab, Abdul Misambano naye ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Sio mie ni moyo.
Tuesday, January 13, 2015
ONYESHO LA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Saada Mohammed akiimba wimbo unaosema "kweli nnae" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja [Picha na Ikulu]
Monday, January 5, 2015
OGOPA KOPA ILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI DAR LIVE

ISHA MASHAUZI KUREKODI WIMBO WA MCHIRIKU
Baada ya kutesa na wimbo wake wa rhumba “Nimlaumu Nani” Isha Mashauzi sasa anajiandaa kuachia ‘single’ nyingine, safari hii ikiwa katika miondoko ya mchiriku.
Akiongea na Saluti5, Isha alisema wimbo huo utakwenda wa jina la “Ado Ado” na utarekodiwa wiki hii kabla ya kauchiwa redioni mwishoni mwa mwezi huu.
“Ni ngoma ya dakika nne ambayo sina shaka kuwa itakimbiza ile mbaya,” alisema Isha.
Isha amesema baada ya kauchia mchiriku, ataachia wimbo mwingine ambao uko katika miondoko ya mutwashi, wimbo ambao umepewa jina la “Usisahau”.
“Lengo langu ni kutoa albam yenye jumla ya nyimbo sita ambayo itakuwa nje kabisa ya miondoko ya taarab, alisema Isha na kuongeza: “Nataka kudhihirisha kuwa nina uwezo wa kuimba aina yoyote ya muziki.”
Friday, December 26, 2014
FIVE STARS YAJA NA TATU MPYA, ISHA MASHAUZI APAKUA SURA SURAMBI
KIKUNDI cha taarab cha Five Stars, ambacho kimezidi kujiimarisha kwa kuwanyakua waimbaji wapya kadhaa, wiki iliyopita kiliingia studio kurekodi vibao vitatu vipya.
Vibao hivyo vipya ni Ubaya hauna soko kilichoimbwa na Mwanaidi Ramadhani, Kishtobe kilichoimbwa na Salha na Sina Gubu kilichoibwa na Mape Kibwana.
Kiongozi wa kundi hilo, Ally J, ametamba kuwa vibao hivyo vitakuwa moto wa kuotea mbali kutokana na kupigwa katika miondoko ya kisasa zaidi.
Wakati huo huo, kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhani, ameachia kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Sura Surambi.
Kibao hicho ni utunzi na uimbaji wake Isha Mashauzi na tayari kimesharekodiwa wikiendi iliyopita kwenye studio za Sound Crafters, zilizoko Temeke jijini Dar es Salaam chini ya producer Enrico.
“Sura Surambi” inategemewa kuendelea kumweka juu Isha Mashauzi kwa namna alivyoimba wimbo huo na hapana shaka itatosha kabisa kuthibitisha ni kwanini alistahili tuzo ya mwimbaji bora wa kike wa taarab.
Gita la solo katika wimbo huo limepigwa na Ramadhani Kalenga, besi limepigwa na Rajabu Kondo wakati kinanda kimepapaswa na Kalikiti Moto.
MBILI MPYA ZA WAKALI WAO MODERN TARADANCE USIPIME
KUNDI la muziki wa taarab la Wakali Wao Modern Taradance limedhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali katika taarab ya kisasa baada ya kuibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Siioni thamani ya pendo.
Kibao hicho kilichotungwa na kuwekwa muziki na kiongozi wa kundi hilo, Thabiti Abdul, kimeimbwa na mwanadada Asia Mariam.
Kibao hicho na kile cha Mtu Mzima hovyo, vimerekodiwa katika studio za Marlon Linje, na vimekolezwa vikorombwezo vyenye mvuto wa aina yake.
Kibao cha Siioni Thamani ya Pendo kimepigwa katika miondoko ya taratibu, ni rhumba fulani lililokwenda shule huku ndani yake kukiwa kumechombezwa vitu fulani kutoka kwa baadhi ya nyimbo maarafu.
Kwa mfano, kipo kipande ambacho kimetoholewa kutoka kwenye wimbo wa Makumbele, uliotamba na bendi ya Orchestra Maquis Original ya hapa nchini zaidi ya miaka 15 iliyopita.
Aidha utakutana pia na vipande kutoka kwa wimbo unaendelea kulitingisha bara la Afrika “Kuchi Kuchi (Oh Baby)” ulioimbwa na J’odie wa Nigeria.
Vibao hivyo vimerekodiwa siku chache baada ya kundi hilo kuzindua albamu yao ya kwanza, inayojulikana kwa jina la Kalieni Viti siyo Umbea”.
OGOPA KOPA WAJA NA TATU KALI MPYA
KUNDI jipya la muziki wa taarab la Ogopa Kopa, linaloongozwa na Malkia wa muziki huo nchini, Khadija Omar Kopa, limedhihirisha kuwa ni tishio baada ya kuibuka na vibao vipya vitatu.
Moja ya vibao hivyo vipya ni Stop Red Card, kilichoimbwa na Anifa Maulid, almaarufu kwa jina la Jike la Chui, mwanadada mwenye sauti murua inayoleta starahamu ya aina yake masikioni.
Kibao kingine ni Chozi la mnyonge, kilichoimbwa na kijana anayechipukia katika muziki huo, Hassan Ali, ambaye amejaliwa kuwa na sauti maridhawa.
Kiongozi wa kundi hilo, Khadija Omar Kopa, naye ameibuka na kibao kikali kinachotarajiwa kubeba jina la albamu mpya ya kundi hilo, Mama mukubwa.
MZEE YUSSUF AJA NA NGOMA MPYA 'MAHABA NIUE'

Ni utunzi na uimbaji wake Mfalme Mzee Yussuf, ngoma kali ambayo inakuwa zawadi nzuri ya kufungia mwaka 2014 na kufungua 2015.
Kazi hii imefanyika katika studio za Sound Crafters, Temeke jijini Dar es Salaam, chini ya producer Enrico. Ndani ya wimbo huu utakutana na mipini mikali ya Mohamed Mauji aliyetambaa vizuri na gitaa lake la solo huku kwenye kinanda kazi kubwa ikiwa imefanywa na Chid Boy.
Kama ilivyo kawaida ya Mzee Yussuf kwenye ngoma ambapo hufunika na vionjo vikali, humu nako ametisha sana, utakutana na vitu vya “Songa Ugali Tule” na vikorombwezo vingine kibao.
Je huu ndio wimbo wa mwisho wa Mzee Yussuf? Sahau kabisa hiyo kitu. Mzee Yussuf ameiambia Saluti5 kuwa lolote linaweza kutokea.
“Ningependa kuacha kuimba mwaka huu, lakini ni mapokeo ya kazi hii ndiyo yatakayoamua, nitaangalia mashabiki wanaipokea vipi, nitaangalia pia namna malengo yangu mengine yatakavyokuwa.
Ninatamani “Mahaba Niue” uwe wimbo wangu wa mwisho, lakini sisemi kuwa huu ni wimbo wangu wa mwisho,” alisema Mzee Yussuf katika maongezi yake na Saluti5
Monday, December 15, 2014
FIVE STARS MODERN TAARAB YAJA KIVINGINE, YAMNYAKUA SALHA, KUZINDUA ALBAMU MPYA DESEMBA 19 DAR
![]() |
| SALHA Aboud |
| MARYAM Aboud |
| MUSSA Kijoti |
| KIONGOZI wa Five Stars Modern Taarab, Ally J (kushoto) |
MWIMBAJI nyota wa taarab nchini, Salha Abdul, amejiunga na kikundi cha taarab cha Five Stars kinachoongozwa na mpiga kinanda mahiri, Ally J.
Salha alitangaza uamuzi wake huo mwishoni mwa wiki kwa kile alichodai kuwa, umelenga zaidi kukuza kipaji chake.
Mwanadada huyo mwenye sura jamali na umbo lenye mvuto alisema amefikia uamuzi huo baada ya kushawishiwa kufanya hivyo na Ally J na pia baada ya kupata barakaa za mama yake mzazi.
"Nilipigiwa simu na Ally J akinieleza kwamba ana mazungumza na mimi na bila kusita nilimkubalia kwa sababu namheshimu sana,"alisema Salha, ambaye kabla ya kujiunga na Five Stars alikuwa kwenye kikundi cha Kings Modern Taarab.
Tayari Salma ameshaibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la Kishtobe, ambacho kimeshaanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya redio nchini.
Kwa mujibu wa Ally J, kikundi hicho kinatarajiwa kufanya uzinduzi wa albamu yake mpya Desemba 19 mwaka huu, utakaofanyika kwenye ukumbi wa Travertine, Dar es Salaam.
Ally J alisema kikundi chake kimeamua kutoka kivingine, ikiwa ni pamoja na kuboresha mipigo yake ya taarab kwa kuweka vionjo vipya kwa lengo la kuleta mvuto kwa mashabiki.
Aliwashukuru wadau mbalimbali wa taarab, ambao wameamua kukiongezea nguvu kikundi hicho ili kiweze kuwa tishio kama ilivyokuwa wakati kilipoanzishwa.
Five Stars ilipata pigo miaka miwili iliyopita baada ya wasanii wake 11 kufariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Morogoro.
All J alisema uzinduzi wa albamu ya kikundi hicho utapambwa na wasanii mbalimbali maarufu wa taarab nchini, wakiwemo wakongwe Khadija Omar Kopa, Mwanahawa Ally na Jokha Kassim.
Kwa upande wake, waimbaji Mussa Kijoti na Maryam Aboud walisema ujio wa albamu yao mpya utakuwa na kishindo kizito kwa vile wameamua kutoka kivingine.
Monday, November 10, 2014
TAARAB YA MIAKA MINNE YA UONGOZI WA DK. SHEIN Z'BAR
Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiwa na Viongozi wengine katika Tamasha maalum la taarab ya kusherehekea miaka minne ya ushindi wa CCM katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani jana.[Picha na Ikulu.]
vikundi mbali mbali vikiburudisha .[Picha na Ikulu.]
Waimbaji wa Kikundi cha Zanzibar Modern Taarab Khadija Khamis na Marium Juma wakiimba wimbo wa Pika Dk.Shein BigUp wakati wa Tamasha maalum la taarab ya kusherehekea miaka minne (4) ya ushindi wa CCM na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, katika Ukumbi wa Salama Hall Bwawani jana [Picha na Ikulu.]
Sunday, October 12, 2014
MWANAHAWA ALLY AMBWAGA KHADIJA KOPA KATIKA NANI MKALI WA RUSHA ROHO
Isha Mashauzi, kiongozi na mwimbaji wa Mashauzi Classic ameshika mkia
MWIMBAJI mkongwe wa muziki wa taarab nchini, Mwanahawa Ally ameibuka mshindi katika shindano la kumsaka mwimbaji bora wa muziki huo.
Mwanahawa, ambaye amewahi kuimbia vikundi mbalimbali vya taarab nchini, aliibuka kidedea baada ya kuwabwaga waimbaji wengine wanne.
Shindano hilo liliandaliwa na blogu ya Rusha Roho, ambayo ni mahsusi kwa ajili ya kuandika habari na makala za wasanii wa muziki wa taarabu.
Katika shindano hilo, Mwanahawa alipata kura sita, ambazo zimepigwa na wasomaji wa blogu hiyo, zikiwa sawa na asilimia 50 ya kura zilizopigwa.
Mwimbaji mwingine mkongwe wa muziki huo, Khadija Kopa alishika nafasi ya pili kwa kupata kura tano, ambazo ni sawa na asilimia 41.
Khadija Yussuf alishika nafasi ya tatu kwa kupata kura nne, ambazo ni sawa na asilimia 33, akifuatiwa na Leila Rashid, aliyepata kura tatu, ambazo ni sawa na asilimia 25. Isha Mashauzi alishika mkia kwa kupata kura mbili, sawa na asilimia 16.
Blogu ya Rusha Roho inawashukuru wale wote walioshiriki kupiga kura za kumtafuta msanii bora wa taarab kati ya wasanii hao watatu.
KHADIJA KOPA 5 (41%)
LEILA RASHID 3 (25%)
ISHA MASHAUZI 2 (16%)
KHADIJA YUSUF 4 (33%)
MWANAHAWA ALLY 6 (50%)
Wednesday, October 1, 2014
MBILI MPYA ZA ISHA MASHAUZI USIPIME
MWIMBAJI nyota wa muziki wa taarab na kiongozi wa kundi la Mashauzi Classic, Isha Ramadhani, ameibuka na kibao kingine kipya kinachokwenda kwa jina la Mapenzi hayana dalali.
Kibao hicho ni mwendelezo wa nyimbo mpya za Isha, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake kipya cha Nimlaumu nani, ambacho amekiimba kwa miondoko ya rhumba, akiimba sauti zote.
Wednesday, September 24, 2014
HIVI NDIVYO VIBAO VIPYA VINAVYOTAMBA MITAANI HIVI SASA
Hammer Q - Kibakuli
Sina Makuu - Ashura Machupa - G5 Modern Taarab...
Hassan Voucher Ft Hasna - Sindano na Golkeeper
Mtu Mzima hovyooo- Wakali wao Modern Taradance
ABDUL MISAMBANO AFUFUKA, AJA NA MPYA ISEMAYO 'SI MIE NI MOYO'
Msanii mkongwe katika muziki wa miondoko ya taarabu nchini, Abdul Misambano, ameibuka na kibao kipya kinachokwenda kwa jina la 'Si mie ni moyo'.
Hii ni mara ya kwanza kwa Misambano kutoa kibao kipya baada ya kuwa kimya kwa miaka kadhaa.
Msanii huyo aliyewahi kung'ara katika kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT Plus), alisema hivi karibuni kuwa, alifanikiwa kurekodi kibao hicho hivi karibuni baada ya kukifanyia mazoezi kwa wiki
kadhaa.
Misambano amesema katika kibao hicho, kinanda kimepigwa kwa umaridadi mkubwa na mkali wa kupapasa ala hiyo, Omary Kisira.
Kwa wanaomkumbuka Misambano, alijipatia umaarufu mkubwa kupitia kibao chake cha Asu kilichotamba miaka ya 1990.
Subscribe to:
Posts (Atom)


































