KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Wednesday, November 25, 2015

ISHA MASHAUZI SASA AJA NA KISMET



Isha Mashauzi “Queen of the Best Melodies” au malkia wa masauti ukipenda, ameingia studio kurekodi wimbo wake mpya kabisa unaokwenda kwa jina la “Kismet”. 

Isha akiwa na kundi zima la Mashauzi Classic, amerekodi wimbo huo katika studio za Sofia Records chini ya producer Ababuu Mwana Zanzibar. 

Huo ni wimbo utakaopatikana katika albam ijayo ya Mashauzi Classic Modern Taarab, ukiachana na “Sura Surambi” inayozinduliwa Alhamisi hii Mango Garden Kinondoni. 

“Hakuna kulala, mwisho albam moja ndiyo mwanzo wa albam ijayo”, alisema Isha Mashauzi katika maongezi yake na Saluti5. 

“Huu ni utaratibu wangu wa siku zote, kuisindikiza albam inayozinduliwa kwa kigongo kitachopatikana albam ijayo,” anafafanua Isha. 

“Kismet” ni utunzi wake Isha Mashauzi ambapo ndani ya wimbo huo, mwimbaji huyo anasema anawawakilisha wale wote ambao wako ndani dimbwi la mapenzi yaliyokolea raha, mapenzi yasiyo na kokoro wala chembe ya maudhi. 

Isha ameiambia Saluti5 kuwa “Kismet” ambayo tayari inatingisha kwenye kumbi za burudani wanazopiga Mashauzi Classic, inaingia hewani wiki hii.
IMETOLEWA KUTOKA BLOGU YA SALUTE 5

Saturday, November 21, 2015

PICHA YA KIHISTORIA KWA WATANZANIA, HAIJAWAHI KUTOKEA NA PENGINE HAITAKUJA KUTOKEA AFRIKA

RAIS John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na marais wastaafu, wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete baada ya kulihutubia na kulizindua jana mjini Dodoma.