KWA HABARI ZA MUZIKI WA TAARAB, WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL ramozaone@gmail.com

Tuesday, January 13, 2015

ONYESHO LA MIAKA 51 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiwa na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo, Said Ali Mbarouk (kulia) Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis.
 Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Pili Seif Iddi (kulia) akiwa na Waziri wa Kilimo na Maliasili, Dk. Sira Ubwa Mamboya
 Baadhi ya wananchi na mashabiki wa Taarab waliohudhuria katika hafla ya Taarab hiyo ya kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Mtumwa Mbarouk akiimba wimbo wa "Mpewa hapokonyeki" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
 Waimbaji wa  Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Asha Alli  na Khamis Nyange, wakiimba wimbo wa Miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, uliotungwa na Profesa Gogo
Mwimbaji wa Kikundi cha Taifa cha Culture Musical Club, Saada Mohammed akiimba wimbo unaosema  "kweli nnae" wakati wa taarab rasmi ya kusherehekea miaka  51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, mbele ya mgeni rasmi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein jana katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja [Picha na Ikulu]

Monday, January 5, 2015

OGOPA KOPA ILIVYOPAGAWISHA MASHABIKI DAR LIVE

 Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Omar Kopa akiimba kwa hisia wakati wa onyesho hilo
 Waimbaji wa Ogopa Kopa wakiwajibika jukwaani wakati wa onyesho hilo
 Mtoto wa Khadija Kopa aitwae Mohammed Kopa akikamua huku nyuma yake akisapotiwa na wenzake
 Mkali wa miondoko ya Kigodoro, Msaga Sumu, akivamia jukwaa na kuwainua mashabiki waliokaa vitini
 Msaga Sumu akimpelekesha Khanifa Khalid anayeserebuka kwa staili ya gwaride
 Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa (kulia) na Khanifa Khalid wakikamua
 Aziza Kimodo akifanya makamuzi wakati wa onyesho hilo
Shad Chotara, mmoja wa waimbaji wa Ogopa Kopa akishusha mpasho wake mpya

ISHA MASHAUZI KUREKODI WIMBO WA MCHIRIKU


Baada ya kutesa na wimbo wake wa rhumba “Nimlaumu Nani” Isha Mashauzi sasa anajiandaa kuachia ‘single’ nyingine, safari hii ikiwa katika miondoko ya mchiriku.

Akiongea na Saluti5, Isha alisema wimbo huo utakwenda wa jina la “Ado Ado” na utarekodiwa wiki hii kabla ya kauchiwa redioni mwishoni mwa mwezi huu.

“Ni ngoma ya dakika nne ambayo sina shaka kuwa itakimbiza ile mbaya,” alisema Isha.

Isha amesema baada ya kauchia mchiriku, ataachia wimbo mwingine ambao uko katika miondoko ya mutwashi, wimbo ambao umepewa jina la “Usisahau”.

“Lengo langu ni kutoa albam yenye jumla ya nyimbo sita ambayo itakuwa nje kabisa ya miondoko ya taarab, alisema Isha na kuongeza: “Nataka kudhihirisha kuwa nina uwezo wa kuimba aina yoyote ya muziki.”